TIMU YA TASSY FC MABINGWA WA MASHINDANO YA IDARA TANGA CEMENT MPIRA WA MIGUU


 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Tanga Cement Diana Malambugi na mgeni rasmi wakati wa Fainali ya mashindano ya Idara ya Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Simba Cement ambaye ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda  hicho Godwin Kamando katikati akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya Tassy Hassani Macho ambao walikuwa mabingwa wa mashindano ya mpira wa miguu  

 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Tassy ambao ni mabingwa kwa upande wa mpira wa miguu Hassani Macho baada ya kuifunga Quary FC mamabo 2-0 mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Saruji mabao yalifungwa na Mustapha Bakari na Nassoro Chande
 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa nahodha wa timu ya Tassy ambao ni mabingwa kwa upande wa mpira wa miguu baada ya kuifunga Quary FC mamabo 2-0 mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Saruji
 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa nahodha wa timu ya Tassy ambao ni mabingwa kwa upande wa mpira wa miguu baada ya kuifunga Quary FC mamabo 2-0 mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Saruji katikati ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda  hicho Godwin Kamando ambaye alikuwa mgeni rasmi


 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano mbalimbali
 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akisalimiana na wachezaji wa timu ya Quary kabla ya kuanza kwa mchezo huo
 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi kulia akisalimiana na wachezaji wa timu ya Tassy FC ambao ni mabingwa wa mashindano ya Idara kwa upande wa mpira wa miguu
 Wachezaji wa timu ya Quary FC wakijadiliana jambo kabla ya kuanza mchezo huo
 TIMU ya Quary wakiwa kwenye picha ya pamoja 
 TIMU ya Tassy ambao ni mabingwa kwa upande wa mpira wa miguuwakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya mchezo huo kuanza

NA MWANDISHI WETU, TANGA.

TIMU ya Tassy FC wametawazwa kuwa mabingwa wapya wa mpira wa miguu mara baada ya kuifunga Quary FC mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali wa Mashindano ya Idara ya kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Simba Cement kilichopo Jijini Tanga.

Tassy wakilabidhiwa Kombe,Mbuzi na Zawadi mbalimbali kutoka kwa mgeni rasmi huku washindi wengine nao wakizawadiwa wakiwemo wa mashindano mengine.

Mashindano hayo ya Idara yalifanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Saruji ambayo yalibeba ujumbe wa wiki ya usalama Tanga Cement kwa mwaka 2019 ni usalama wao, usalama wa familia yako.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa licha ya Tassy kutawala kuanzia kipindi cha pili huku wakicheza kwa umakini mkubwa ambao ulipelekea kuandika mabao hayo mawili.

Bao la kwanza lilipatikana kwenye dakika ya 44 kupitia Mustapha Bakari ambayo alitumia uzembe wa mabeki wa wapinzani wao kupachika wavuni bao hilo.

Baada ya kuingia bao hilo wapinzani wao Quary FC waliweza kurudi kujipanga na kulishambulia lango la Tassy FC bila mafanikio kutokana na wachezaji wao kupiga mashuti yaliyokuwa yakienda nje ya lango.

Kutokana na shambulio hilo timu ya Tassy FC walirudi kujipanga na kuanza kucheza pasi fupi fupi na ndefu na hivyo kufanikiwa kuandika bao la pili ambalo lilifungwa na Nassoro Chande kwenye dakika ya 78.

Akizungumza wakati akifunga mashindano hayo Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Simba Cement Godwin Kamando aliwataka michezo husaidia kuwaweka watu pamoja na kuweza kubadilishana uzoefu hivyo ni muhimu.

Kamando alisema kupitia michezo wanaweza kuimarisha miili yao ikiwemo kuwaepusha na madhara yanayoweza kutokana na watu kutokufanya mazoezi .

Naye kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Simba Cement Diana Malambugi aliwapongeza wachezaji ambao wamefanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Alisema wafanyakazi kushiriki kwenye michezo ni jambo muhimu sana kwani lina imarisha miili yao na kuweza kuongeza hari katika utekelezaji wa majukumu yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527