SHIRIKA LA LIFEWATER INTERNATIONAL LAZINDUA MRADI WA MAJI MKOANI SHINYANGA




Shirika la Lifewater International lenye makao yake makuu nchini Marekani limezindua mradi wa maji mkoani Shinyanga, ambapo katika awamu ya kwanza utatekelezwa katika kata tatu za Mwantini, Mwamala pamoja na Mwalukwa zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


Uzinduzi wa mradi huo wa maji umefanyika leo, Oktoba 25, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo,Mboneko  amelipongeza Shirika la Lifewater International, kwa kuanzisha mradi wa maji mkoani Shinyanga ambao utaanza kutekelezwa kwenye kata hizo tatu za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambazo zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji safi na salama.

Amesema Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli inasisitiza sana upatikanaji wa maji kwenye maeneo mengi ili wananchi waweze kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama, pamoja na kuugua magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji ambayo siyo salama kiafya, na kubainisha mradi huo upo sehemu sahihi.

“Tunalishukuru sana Shirika hili la Lifewater International kwa kutuletea mradi huu wa maji mkoani Shinyanga, na kuanza kutekelezwa kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo tunaomba mradi huu pia ufike na kwenye maeneo mengine ambayo yana shida ya maji safi na salama ikiwemo wilaya ya Kishapu,”amesema Mboneko.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Lifewater International Tanzania Devocatus Kamara, amesema mradi huo kwa kuanza utatekelezwa kwenye kata hizo tatu za halmshauri ya wilaya ya Shinyanga, ambazo ni Mwantini, Mwamala na Mwalukwa , na baada ya hapo utapanuka kwenye maeneo yote ya mkoa wa Shinyanga na mikoa mingine, ambayo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama na usafi wa mazingira.

Amesema mradi huo utadumu kwa muda wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2020 hadi 2024 na utagharimu kiasi cha Shilingi za kitanzania 4,286,070,528, ambao utajenga visima vipya virefu vya maji safi na salama na kuvikarabati vibovu, kujenga na kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora, kuboresha usafi wa mazingira, na utahamasisha na kuhimiza ushiriki wa jamii kikamilifu ili kuhakikisha uendelevu wa mradi.

Kwa upande wake,Meneja wa Shirika  Lifewater International mkoa wa Shinyanga Benety Malima, amesema kuwa katika maeneo  ambapo maji ya ziwa Victoria yamekwishafika, watafanya utaratibu wa kuendelea kuyasambaza katika maeneo yanayokusudiwa.

Pia amesema maeneo ambayo yatapitiwa na mradi huo wa maji, ni sehemu za shule, zahanati, pamoja na kwenye makazi ya watu, ambapo mradi huo umelenga kufikia watu 100,000.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizindua mradi wa maji wa Shirika la Lifewater ambao utatekelezwa mkoani Shinyanga na kuanza kutekelezwa kwa awamu ya kwanza katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga katika Kata tatu za Mwantini, Mwamala na Mwalukwa, ambao utadumu ndani ya miaka mitatu (2020-2024). Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Shirika  la Lifewater International Tanzania Devocatus Kamara, akielezea namna mradi huo wa maji utakavyofanya kazi Mkoani Shinyanga.

Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akiwataka watumishi wa Serikali kutoa ushirikiano kwenye utekelezaji wa mradi huo wa maji.

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.

Uzinduzi ukiendelea.

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.

Kushoto ni Meneja wa Lifewater International mkoa wa Shinyanga Benety Malima akiwa kwenye kikao cha uzinduzi wa mradi wao wa maji.

Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akichangia mada kwenye kikao cha uzinduzi wa mradi wa maji kutoka Shirika la Lifewater Internationali.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini mkoa wa Shinyanga (Ruwasa) Malwa Kisibo,akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi huo wa maji.

Kaimu meneja wa wakala wa maji vijijini wilaya ya Shinyanga (Ruwasa) Emaeli Nkopi, akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi huo wa maji.

Kaimu Afisa afya mkoa Mussa Makungu akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi huo wa maji kutoka Shirika la Lifewater International.

Kaimu Afisa afya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Gibril Mongi akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.

Kaimu mganga mkuu wa halmshauri ya wilaya ya Shinyanga Bashiri Salumu akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi maji kutoka Shirika la Lifewater Intenational.

Wajumbe wakipiga picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko aliyekaa kwenye kiti katikati mara baada ya kumaliza kuzindua mradi wa maji kutoka Shirika la Lifewater International.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527