MAHAKAMA KUU YAKUBALI ACT- WAZALENDO KUJIUNGA KWENYE KESI KUHUSU UKOMO WA URAIS | MALUNDE 1 BLOG

Friday, October 25, 2019

MAHAKAMA KUU YAKUBALI ACT- WAZALENDO KUJIUNGA KWENYE KESI KUHUSU UKOMO WA URAIS

  Malunde       Friday, October 25, 2019

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekubali ombi la Chama cha ACT-Wazalendo kujiunga kama washtakiwa kwenye kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Dezydelius Mgoya, maarufu kama Mkulima, kuhusu ukomo wa urais.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Dk. Benhaj Masoud baada ya kusikiliza maombi ya ACT-Wazalendo kujiunga na kesi hiyo kwa sababu wana maslahi nayo.

Wakili wa ACT-Wazalendo, Jebra Kambole, alidai kuwa mteja wake ameomba kujiunga kwa sababu ni chama kilichosajiliwa na kimeshiriki katika uchaguzi.

Pia alidai kuwa chama hicho kina wanachama Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar kwa mujibu wa matakwa ya kisheria na kikatiba.

Mgoya alifungua kesi hiyo chini ya kifungu cha 4 cha sheria ya utekelezaji haki na wajibu, sura ya 3 ya mwaka 1994 chini ya Ibara ya 30(3) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Mgoya anahoji Ibara ya 40(20) ya Katiba ambayo imeweka ukomo wa mihula miwili tu ya miaka mitano mitano ya uongozi katika nafasi hiyo ya urais.

Hivyo anaiomba mahakama hiyo itoe tamko na tafsiri ya maana sahihi na athari za masharti ya ibara hiyo.Pia anaiomba mahakama itoe tafsiri ya maana dhahiri ya masharti ya Ibara ya 42(2) ya Katiba kwa kuhusianisha na masharti ya Ibara za 13, 21 na 22 za Katiba hiyo.

Kadhalika, Mgoya anaiomba mahakama itoe tafsiri ya maana ya Ibara hiyo ya 40(2) kwa kuhusianisha na Ibara ya 39 ya Katiba.

Credit:Nipasahe


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post