LUSINDE: KIJANA MDOGO,UNA MIAKA 22,HUNA KAZI YA UHAKIKA,HUNA MSHAHARA LAKINI UNA MADEMU WANNE ,WEWE NI TATIZO


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mbunge wa jimbo  la Mtera mkoani Dodoma Livingstone Lusinde amewataka vijana kote nchini kujitathimini na kuachana na masuala ya anasa ikiwa ni pamoja na Umalaya na badala yake wawajibike katika kazi za kuwaletea maendeleo. 


Mhe.Lusinde amesema hayo jijini Dodoma akiwa mgeni Rasmi katika kongamano la  Vijana Mkoa wa Dodoma lililolenga kujadili mchango wa  Baba wa Taifa Mwl.Julus  Kambarage Nyerere ikiwa  taifa la Tanzania likifanya kumbukizi ya Miaka 20 tangu afariki dunia  mwaka 1999. 


Mbunge huyo amesema vijana wa siku hizi wamekuwa wakifanya masuala ya Umalaya na ukahaba na mambo mengine ya anasa wakiwa wadogo na kushinda baa badala ya kuwajibika katika kazi hivyo wanapaswa kubadilika. 


“Kijana Mdogo,una miaka 22,huna kazi ya uhakika,huna mshahara lakini una mademu wanne ,wewe ni tatizo,shida ni wewe,piga hela zote ulizotoa Guest na chipsi ni mtaji.Wewe ni tatizo kubwa,huwa ninaangalia sana mitaala ya elimu,wakati mwingine watoto tunawafundisha ujinga.Alisema. 


Mhe.Lusinde amesema kuna baadhi ya mambo vijana wanatakiwa kujitathimin na kufanya mambo makubwa na kwa kasi na kuacha kupoteza muda kupoteza fedha kwa kujiunga internet na kuchati kwenye Magroup ya Whatsaap yasiyokuwa na tija kwani ni kupoteza muda na badala yake watumie miundombinu iliyoachwa na   Mwalimu Nyerere katika kuwaletea Maendeleo. 


“Lazima kuna baadhi ya vitu unapaswa kugundua na kung’amua,lazima miundombinu tuifanyie kazi katika kutuletea maendeleo,kuna mambo mengine yanahitaji haraka,mtu anakwambia polepole ndio mwendo na wewe unakubali.huna shughuli,huna mshahara lakini una simu tatu unachati group hili hadi lile,wewe ni Poyoyo.Amesema. 


Hata hivyo,Mhe.Lusinde amewaasa  Vijana kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kupambana na rushwa kwani rushwa hunyonya haki ya mtu. 


Aidha,Mhe.Lusinde amewataka vijana kujiandaa mapema pindi wanapotaka kufanya maendeleo na akatolea mfano mwanafunzi anayefaulu vizuri mtihani ni Yule aliyejiandaa mapema katika  na kudai kuwa ng’ombe hanenepi siku ya mnada. 


Kwa upande wake katibu wa  Vijana mkoa wa Dodoma Joel Makwaia  amesema Mwl.Nyerere alikuwa kiongozi Mzalendo wa Taifa na alijitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha taifa linasonga mbele.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527