CHINA YAADHIMISHA MIAKA 70 YA KUANZISHWA KWAKE KWA KUZINDUA KOMBORA LA NYUKLIA LINALOWEZA KUFIKA MAREKANI KATIKA MUDA WA DAKIKA 30 | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 1, 2019

CHINA YAADHIMISHA MIAKA 70 YA KUANZISHWA KWAKE KWA KUZINDUA KOMBORA LA NYUKLIA LINALOWEZA KUFIKA MAREKANI KATIKA MUDA WA DAKIKA 30

  Malunde       Tuesday, October 1, 2019

Leo Oktoba Mosi, Mkutano wa kuadhimisha miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na gwaride kubwa la jeshi na umma limefanyika katika Uwanja wa Tian'anmen katikati ya mji wa Beijing.


Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti, rais na katibu mkuu wa Kamati kuu ya kijeshi ya China Xi Jinping, ametoa hotuba  na kukagua gwaride. 

Amesisitiza kuwa katika miaka 70 iliyopita, kutokana na kuwa na imani ya pamoja na jitihada za pamoja, watu wa China wamepata mafanikio makubwa yanayong'ara kote duniani. 

Rais Xi amesisitiza kuwa China imesimama kidete mashariki mwa ulimwengu, na hakuna nguvu yoyote inayoweza kuyumbisha hadhi ya China, na kuwazuia watu wa China na taifa la China kupiga hatua. 

Kwenye hotuba yake, rais Xi amesema kuwa kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China miaka 70 iliyopita, kulibadilisha kikamilifu hatma ya China iliyokuwa maskini, dhaifu na kunyanyaswa, na kufungua njia ya kuelekea ustawi mpya wa taifa la China.

Rais Xi amesisitiza kuwa katika mchakato wa kusonga mbele, China inapaswa kushikilia uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, kutoa kipaumbele kwa maslahi ya umma, kutekeleza kikamilifu nadharia, mipango na mikakati ya Chama, kuendelea kukidhi matarajio ya umma kwa maisha bora, na kuendelea kupata mafanikio mapya ya kihistoria. 

Gwaride hilo lilihusisha wanajeshi 15,000, vifaru 580 na mifumo mingine ya silaha pamoja na makombora ya masafa marefu.  


Miongoni mwa makombora hayo ni kombora la Dong Feng 41 (DF 41) lenye uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia. Linauwezo wa kutua popote Duniani huku likitumia dakika 30 tu kufika Marekani.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post