MBUNGE AZZA ATOA MSAADA WA TANKI LA MAJI KWA AJILI YA CHOO CHA WANAFUNZI WA KIKE SHULE YA SEKONDARI SAMUYE | MALUNDE 1 BLOG

Friday, October 4, 2019

MBUNGE AZZA ATOA MSAADA WA TANKI LA MAJI KWA AJILI YA CHOO CHA WANAFUNZI WA KIKE SHULE YA SEKONDARI SAMUYE

  Malunde       Friday, October 4, 2019

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 2000 kwa ajili ya kuwekea maji kwenye choo cha wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Samuye iliyopo katika wilaya ya Shinyanga.

Azza amekabidhi tenki hilo la maji leo Ijumaa Oktoba 4,2019 wakati wa mahafali ya  15 ya Kidato cha Nne 2019 ambapo Jumla ya wanafunzi 94 wamehimu elimu ya kidato cha nne.

Msaada huo wa tenki la maji kusaidia watoto wa kike katika shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi  494 unatokana na kuridhishwa kwa mbunge huyo kutokana na jitihada zilizofanywa na wazazi na walezi wa wanafunzi katika shule hiyo kujitolea kujenga matundu 22 ya vyoo ambapo 11 ni kwa ajili ya wavulana na 11 wasichana.


Katika hotuba yake,Mhe. Azza amewataka wanafunzi kuzingatia masomo yao na kuepuka vishawishi vinayoweza kusababisha kupata mimba ama kuolewa wangali wadogo.

"Nimeambiwa mwaka huu 2019 katika shule hii mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu amepata ujauzito naomba watoto wa kike muepuke vishawishi vinavyoweza kufanya mkatishe ndoto zenu",alisema Azza.


"Shule hii ipo karibu na barabara ya lami,nawasihi wanafunzi muachane na lifti za magari, nanyi wazazi naomba mrudishe utaratibu wa wanafunzi kutumia baiskeli au kama ni mwendesha bodaboda anayebeba mwanafunzi basi ajulikane badala ya kila mwendesha bodaboda kubeba mwanafunzi",aliongeza Azza.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi tenki la maji lenye ujazo wa lita 2000 kwa ajili ya kuwekea maji kwenye choo cha wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Samuye iliyopo katika wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye Mahafali ya Kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Samuye iliyopo katika wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akifurahia jambo na wanafunzi wa kidato cha nne kwenye Mahafali ya Kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Samuye iliyopo katika wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha na wahitimu wa kidato cha nne.
Wahitimu wa kidato cha nne Shule ya sekondari Samuye

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post