WANAWAKE 15 WAINGIA NDANI YA 18 YA RPC MUROTO KWA KUFANYA UKAHABA


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

JESHI la Polisi mkoani Dodoma limewakamata na kuwafikisha mahakamani makahaba 15 ambapo wamehukumiwa kifungo cha miezi sita kila moja huku wanaume wanne waliosadikiwa kuwa ni wateja wao wakiachiwa baada ya kukosekana kwa ushahidi.


 Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto alisema  katika msako wa Septemba 2, mwaka huu saa tatu kamili usiku mtaa wa Uhindini walikamatwa wanawake 15 wakifanya biashara ya ukahaba na kuhatarisha amnai na utulivu katika mtaa huo kinyume na kifungu 176 (a) (f) (g) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo 2002.

 Alisema washtakiwa walifikishwa mahakamani, walisomewa mashtaka na ushahidi dhidi yao ulitolewa na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kila moja bila kulipa aini.

Alisema msako mwingine umefanyika wamekamatwa makahaba saba na watafikishwa mahakamani  AlisemaAlisema makahaba hao waliona fursa ya kuja kufanya matukio ya ngono kitendo ambacho hakikubaliki.

Sasa hivi wako gerezani Isanga wamepokelewa kwa ajili ya nguvu kazi, wataponda kokoto na kufanya kazi nyingine” alisema . Alisema  msako huo utakuwa endelevu. 

Makahaba waliohukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani wametakjwa kuwa ni  Suzana Onesmo (27), Mariam Omary (29), Maimuna Issa (38), Bhoke Chacha (30), Swaumu Bakari (26),  Rahma Abdi (28), Magreth Humphrey (27),  Wema Saidi (25),  Jeniffer Wilson (33), Lydia Kilale (30),  Manka Richard (21),  Mwasuma Hassan (26),  Angel Joseph (29), Zaina ramadhani (30) na Tatu Saidi (27). Katika tukio linguine kamanda  Muroto alisema zilikamatwa silaha mbili zikimilikiwa kinyume cha sharia.

 Alisema Agosti 18, mwaka huu katika mtaa wa mazengo kata ya Zuzu, alikamatwa Baraka mgomochi (24), mkazi wa Nkuhungu akiwa na silaha aina ya bastola muundo wa bereta yenye namba AR- 3648-1981 yenye usajili wa TZC 68344 ikiwa na magazine ambayo haina risasi.

 Alisema mtuhumiwa alifukia  silaha hiyo pembeni ya karo la choo na uchunguzi ulifanyika na kubaini silaha hiyo iliibiwa Kurasini Jijini Dar es salaam baada ya watuhumiwa kuvunja nyumba na kuiba.

Katika tukio linguine alisema lilitokea Ilangali, wilaya ya chamwino mkoani hapa, Jeshi la polisikwa kushirikiana na askari wa wanyamapori kutoka mkoa wa Iringa alikamatwa John Gabriel (53) akiwa na silaha aina ya Gobole yenyemba DA 827-08 akiwa anaimiliki kinyume cha sharia na akiitumia kinyume cha sharia kwa uwindaji haramu wa wanyamapori.

Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

 Alisema katika msako dhidi ya wavunjaji, wezi, wanaohifadhi mali za wizi, wamekamatwa watuhumiwa wane kwa makosa hayo

 Alisema katika eneo la mailimbili alikamatwa Juma Ally (22),  Joseph Mapunda (28) mkazi wa Sawswa wakiwa na spika tatu kubwa na stendi ya mixer moja mali ambazo ni za wizi.

 Katika eneo la kizota alikamatwa Almando David (19), mkazi wa kizita akiwa na jumla ya televisheni nne aina ya Philips, nchi 30, Tv aina ya Aborder inchi 32, Sony nchi 18 na LG nchi 21 akihifadhi huku akijua ni mali za wizi.

Alisema katika eneo la Ntyuka alikamatwa Allen Jonathan (28) fundi ujenzi akiwa na mabati matano ambayo ni mali ya wizi.

 Pia alisema katika eneo la Changombe na maili mbili walikamatwa watuhumiwa 69 waliokuwa wakitafutwa kwa makosa mbalimbali, pia zimekamatwa bajaji mbili, pikipiki 22, laptop kompyuta mbili na kisu kimoja.

 Alisema watuhumiwa watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post