UTEUZI MPYA ULIOFANYWA NA RAIS MAGUFULI LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Chamriho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Uwekezaji wa Mapato ya Mafuta na Gesi (Portfolio Investment Advisory Board).


Dkt. Chamriho ni Katibu Mkuu wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti, Rais Magufuli amewateua wajumbe wanne wa bodi hiyo ambao ni;
  1. Casmir Sumba Kyuki (Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria).
  2.  Dkt. Suleiman Magesa Missango (Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya Tanzania – BOT).
  3.  Safiel Fahamuel Msomvu (Kaimu Meneja Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania – TPDC).
  4.  Dkt. Mussa Daniel Budeba (Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Chamriho na Wajumbe hao umeanza tarehe 25 Septemba, 2019.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527