TIGO YAZINDUA HUDUMA YA ‘OFFICE INTERNET’ KWA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKATI TANZANIA


Afisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft 
Kaimu mkuu wa mauzo-Nick kazuka akifanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya. uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft 
Afisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani akimkabidhi Router Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo. mara baada ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao makuu ya ofisi za Tigo Jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao makuu ya ofisi za Tigo Jijini Dar es salaam.
Mtaalam bidhaa Tigo Business Brian Swai akifafanua jambo kwa wageni waalikwa uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao makuu ya ofisi za Tigo Jijini Dar es salaam.

  • Ni huduma ya intaneti yenye kasi inayokwenda sambamba na mfumo wa kisasa wa kibiashara kutoka Microsoft 
Dar es Salaam: Septemba 12, 2019, Kampuni ya simu ya Tigo, kupitia kitengo chake cha Tigo Business leo imetangaza rasmi uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft . Hatua hii inazidi kuifanya Tigo kuendelea kuwa kinara wa ubunifu kuiwezesha kampuni katika kujitolea kufanya biashara zake kwa malengo. 
Sambamba na uzinduzi wa  huduma ya ‘Home Internet’ uliyofanywa na Tigo hivi karibuni,  huduma ya ‘Office Internet’ inakuja na faida endelevu kwa wateja wenye biashara ndogo na za kati ambao hupendelea huduma za intaneti kwa mkataba. Hii inadhihirisha matumzi bora ya mtandao wa wenye kasi nchini Tanzania wa 4G+. 

Afisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani, aliwaambia wateja wa Tigo kuwa, kwa sasa wana uwezo wa kutoa huduma bora zinazoendana na wakati kwa kushirikiana na wataalamu wa Microsoft. “Tulifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu sana na wateja wetu, ambapo walituonyesha maeneo matatu muhimu yenye changamoto; Muda unaotumika kuunganisha huduma ya intaneti, Kasi ya huduma hiyo na ukosefu wa maana halisi,  Matumizi ya intaneti na zana zenye uhusiano na biashara. Tuna furaha kutangaza kuwa, ‘Office Internet ina huduma ya daraja la kwanza iliyounganishwa na mtandao wa Tigo 4G+,  wenye watumiaji wengi duniani kote chini ya ushirikiano wa Microsoft.
Huduma hii kwa ujumla wake inatumika bila muunganisho wa waya, kwa maana ya kwamba mteja wetu anatakiwa kuwasha kifaa chake cha Modem  au Router. Ofisi ya mteja inaweza kuunganisha vifaa 10 hadi 32 kwenye inteneti kwa mara moja. Microsoft 365 inaruhusu kufanya mambo mbalimbali ikiwamo utumaji wa barua pepe za kibiashara,  Kutuma na kuhifadhi ujumbe katika mtandao, Matumizi ya Microsoft katika masuala yote ya kibiashara ikiwamo mikutano ya moja kwa moja mtandaoni 
Kujiunga na huduma ya ‘Office Internet’ tembelea duka lolote la Tigo nchini ili kujisajili. Wateja wanaotumia huduma hii watapewa kipaumbele katika huduma kwa wateja. Kwa nyongeza, mteja anaweza pia kupiga  0711100101 au barua pepe Tigobusiness@tigo.co.tz.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527