MIMEA INAYOKULA NYAMA YAANZA KUPANDWA TENA....INA MIKONO MINGI YA KUKAMATIA MSOSI

Mimea inayokula nyama iliyopo hatararini kuangamia imeanza kupandwa tena katika maeneo kadhaa ya Uingereza katika jaribio la kupunguza kuangamia kwake.


Wataalam wa mimea wanasema kwamba mimea hiyo iliyo na umbo la kuvutia imetoweka katika maeneo mengi kutokana na uhaba wa maeneo yenye ardhi zenye unyevu.

Ikiwa na mikono inayoshika na kula wadudu, mmea huo ni mmojawapo ya makumi ya mimea inayokula nyama Uingereza.

Charles Darwin alifurahishwa sana na spishi ya mmea huo , na hivyo basi kukusanya picha na vipimo katika kitabu chake kwa jina Insectivorous Plants, kilichochapishwa 1876.

Anasema kwamba alipendelea sana kuhusu mmea kwa jina Drosera, unaofahamika kama Dawy kwa lugha ya Latin ikilinganishwa na kitovu cha spishi zote duniani.

Ni spishi ilio nadra kupatikana kulingana na Joshua Styles kutoka chuo kikuu cha Cheshire, ambaye alianzisha hisani yake ya hifadhi kwa jina North West Rare Plant Initiative kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

Nchini Uingereza mmea huo umeorodheshwa kama ulioangamia na hupatikana chini ya maeneo 20 hivyo basi kutopatikana kwake na hali yake kulinishawishi kutaka kuupanda tena.Joshua Styles kushoto) akibeba mbegu ya mmea wa Sundew
Je mmea huo ni upi na unapatikana wapi?

Ulikuwa ukipatikana kwa wingi nchini England , mmea huo ulianza kuangamia katika karne iliopita.

Mabadiliko ya matumizi ya ardhi yamesababisha kukauka kwake katika maeneo yanye ardhi zilizo na unyevu.

Je mmea huo unazinduliwa vipi upya?

Joshua Styles alifanikiwa kupanda mmea huo kutokana na majani yaliyokatwa yaliyotoka katika mimea michache iliyosalia ambayo imeweza kustahimili mazingira magumu katika eneo la Cumbria.

Alizindua mimea aina 10 katika eneo la Rsley Moss karibu na Warrington, akishirikiana na wakfu wa Chesser na ule wa wanyama pori wa Lancashire.

Mmea huo unaokula nyama unafaa kustahimili katika mazingira hayo na kuanza kuzaana.

''Kila mwaka wakati unapotoa maua unatoa makumi ya maelfu ya mbegu ndogo ndogo zinazofanana na vumbi'' , alisema.

Unapopanda 10 haionekani kama ni mingi, bali idadi ya mbegu zinazotolewa , ''ninatumai kupata mbegu nyingi mwaka ujao.Sundew ndio mimea ya kwanza inayokula nyama kufanyiwa utafiti na kumvutia Charles Darwin
Mmea wa Sundew (Drosera anglica)

Kawaida mimea hujipatia chakula kutoka kwa mchanga kupitia mizizi yao, lakini mimea inayokula nyama imepiga hatua ya kula protini za wanyama.

Mmea huo, una 'mikono' mingi midogo midogo inayotoa maji yenye harufu tamu ambayo huwavutia wadudu.

Mikono hiyo midogo baadaye huwashika wadudu hao na kuwakamua ndani ya majimaji hayo yanayonata.

Enzymes za mwilini hujitokeza polepole na kuwavunja wadudu hao kuwa chakula chenye virutubishi.Wadudu huvutiwa na majani ya mmea huo.

Mtunzaji huyo mdogo alivutiwa na utaalamu wa mimea akiwa na umri wa miaka saba, na amekuwa akisoma mimea tangu hapo.

Anasema ni muhimu kuhifadhi mimea ya kula nyama kwa faida yao kwa mazingira na viumbe hai, na kwa faida yao ya baadaye, kama vile chanzo kinachoweza kutengeneza dawa mpya.
CHANZO - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527