MFANYAKAZI CRDB AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMUIBIA MTEJA ZAIDI YA MILIONI 100 | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 28, 2019

MFANYAKAZI CRDB AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMUIBIA MTEJA ZAIDI YA MILIONI 100

  Malunde       Saturday, September 28, 2019

Ofisa  wa benki ya CRDB tawi la Ubungo,Andrew Babu(27)na wenzake watatu ambao ni Wafanyabiashara wamefikishwa katika Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar  wakikabiliwa tuhuma za Uhujumu Uchumi ikiwamo kula njama,kugushi tembo kadi, wizi na kutakatisha zaidi ya Mil 100.Mbali na Babu, washitakiwa wengine ni William Sige, Justina Boniphas na Ally Tatupa ambao wote wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 101/2019.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliwasomea mashtaka yao Alhamisi Septemba 26, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Agustina Mbando.Hakimu Mmbando ameahirisha kesi hiyo hadi  Oktoba 10, 2019 itakapotajwa tena.

Washtakiwa wote walirudishwa rumande kutokana na shtaka la utakatishaji fedha kutokuwa na dhamana.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post