Picha : DC MBONEKO AONGOZA WANANCHI KUFANYA MAZOEZI SHINYANGA


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko ameongoza wakazi wa Shinyanga kufanya mazoezi leo Jumamosi Septemba 14,2019 ikiwa sehemu ya utaratibu waliojiwekea wa kufanya mazoezi kila Jumamosi ya pili ya kila mwezi na Jumamosi ya mwisho ya kila mwezi.

Mazoezi hayo yakiongozwa na Kauli mbiu 'Afya yangu,Mtaji Wangu' yameanzia katika Viwanja vya Sabasaba Kambarage na kuishia katika Viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa,taasisi,mashirika na wadau wa michezo na afya.

Akizungumza wakati wa mazoezi hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko amesema wataendelea na utaratibu wa kufanya mazoezi ya pamoja kila Jumamosi ya kila mwezi lakini pia Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi huku akiwashauri wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi kila siku ili kuimarisha afya zao.

"Leo ni Jumamosi ya pili katika mwezi huu,Nawashukuru mliojitokeza kuungana nasi katika mazoezi haya.Kwa kweli hili ni agizo la serikali kufanya mazoezi.naomba tuendelee na mazoezi kwa ajili ya faida yetu,niombe kwa wenye uwezo kuna Gym yetu ambapo mchango kwa mwezi ni 3,000/= na kama hiyo hamuwezi basi kila siku tufanye mchaka mchaka,tukimbie,tutembee kwa saa nzima kwa ajili ya afya zetu",amesema Mboneko.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa mazoezi ya pamoja leo Jumamosi Septemba 14,2019 katika Viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa mazoezi ya pamoja leo Jumamosi Septemba 14,2019
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa mazoezi ya pamoja leo Jumamosi Septemba 14,2019
Viongozi na wananchi wakiwa katika Viwanja vya Shycom
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akielezea faida za kufanya mazoezi wakati wa mazoezi ya pamoja leo Jumamosi Septemba 14,2019 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akiongoza mazoezi ya kukimbia leo Jumamosi Septemba 14,2019.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527