KAMPUNI YA ENGEN YAFUNGUA VITUO VIWILI JIJINI MWANZA


Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kampuni ya Engen inayohusika na uuzaji wa mafuta na vilaini mbalimbali vya vyombo vya moto ikiwemo magari na pikipiki, imewasogeza karibu huduma wateja wa mikoa ya Kanda ya Ziwa baada ya kufungua vituo viwili vya mafuta jijini Mwanza.

Ufunguzi wa vituo hivyo ambavyo ni Engen Sinai pamoja na Engen Mkuyuni umefanyika Septemba 25, 2019 na kutoa fursa kwa wateja kunufaika na ofa mbalimbali ikiwemo mafuta, jaketi za usalama barabarani, kofia pamoja na tisheti.

Baada ya kufanya ufunguzi rasmi wa vituo hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato alisema tayari vituo 10 vya Engen vimefunguliwa katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Arusha na Dodoma ambapo matarajio ni kuwa na vituo 20 ifikapo mwaka 2020.

Muhato alisema lengo la kampuni ya Engen ni kuendelea kutoa huduma bora za vilainishi na mafuta yasiyochakachuliwa kwa wateja wake huku wakiwa na uwanda mpana wa kufanya malipo kwa mfumo wa taslimu, M-Pesa, kadi za benki pamoja na kadi za Engen.

Aidha aliongeza kwamba wateja wa Engen wataendelea kunufaika na ofa na huduma mbalimbali za bure ikiwemo mteja kusafishiwa gari, kujaziwa upepo pamoja na ushauri wa aina gani ya vilainishi bora vinafaa gari lake.

Naye Ruben Petro ambaye ni mmoja wa waendesha bodaboda jijini Mwanza aliyenufaika na ofa za Engen baada ya ufunguzi wa kituo cha mafuta Engen Mkuyuni, aliishukru kampuni hiyo kwa kusogeza karibu huduma zake huku ikiwajali kwa ofa mbalimbali na hivyo kuwasihi wateja wengine kuchangamkia huduma za kampuni hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo cha mafuta Engen Mkuyuni.
 Shangwe na vigeregere baada ya ufunguzi wa kituo cha mafuta Engen Mkuyuni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (kulia) akimjazia mafuta bure mmoja wa waendesha bodaboda jijini Mwanza.
 Waendesha bodaboda jijini Mwanza wakinufaika na mafuta bure baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha mafuta cha Engen Mkuyuni jijini Mwanza.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha mafuta Engen Sinai jijini Mwanza.
 Shangwe baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha mafuta Engen Sinai jijini Mwanza.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (kulia) akimpongeza mmoja wa waendesha bodaboda waliofika katika kituo cha Engen Sinai kunufaika na huduma za Engen.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (kulia) akimjazia bure mafuta mmoja wa waendesha bodaboda jijini Mwanza baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha Engen Sinai.
 Ukifika kituo chochote cha Engen, utanufaika na huduma mbalimbali ikiwemo gari kusafishwa.
Tazama Video hapa chini





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527