WAZIRI MWAKYEMBE AAGIZA KUSAKWA KWA WASHEREHESHAJI WA HARUSI 'MA MC' WASIO NA VITAMBULISHO

Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika mkutano na wadau wa sekta ya habari Utamaduni, Sanaa na Michezo uliofanyika leo katika ukumbi wa mkoa uliopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. 

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog

Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa agizo la kuwasaka kubaini na kuwakamata washereheshaji wa harusi maarufu kama MC mkoani Kagera ambao hawana vitambulisho vya kazi hiyo na kuwa atakayebainika atachukuliwa sheria kali ikiwemo harusi hiyo kusimama wakati huo.

Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo, Agosti 30,2019 wakati akiwa mkoani Kagera katika mkutano na wadau wa sekta ya habari Utamaduni, Sanaa na Michezo uliofanyika katika ukumbi wa mkoa uliopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa tayari serikali imeishaweka utaratibu wa kila mfanyabiashara kuwa na kitambulisho na kudai kuwa utaratibu huo unajulikana nchi nzima.

Ameeleza kuwa kitendo cha baadhi ya washereheshaji kunyonya jasho la ambao tayari wamelipia vitambulisho vya kuwatambua katika kazi hiyo ni kosa kisheria.

Waziri huyo amesema ni jambo la kusikitisha na kutoa agizo la Wakaguzi kufanya msako mkali ili kubaini washereheshaji ambao hawajasajiriwa na kuwa wakibainika watachukuliwa sheria kali ikiwemo harusi hiyo kusimamishwa wakati huo. 

Amesema sambamba na kuwachukulia sheria kali watatozwa faini itakayoingizwa katika mfuko wa wasanii ili kuinua tasnia ya utamaduni na sanaa.

Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika mkutano na wadau wa sekta ya habari Utamaduni, Sanaa na Michezo uliofanyika katika ukumbi wa mkoa uliopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.Picha zote na Lydia Lugakila - Malunde1 blog

Wadau wa sekta ya habari, utamaduni,Sanaa na michezo wakiwa ukumbini.


Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akipokelewa mkoani Kagera leo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527