TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO WA 50 WA CPA


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt Ally Mohamed Shein Anatarajiwa  kuwa mgeni Rasmi katika mkutano mkubwa wa 50 wa chama cha Mabunge cha  Jumuiya ya Madola, Kanda ya Afrika .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Agosti 22,2019, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai amesema wageni mbalimbali wamealikwa ikiwemo Maspika kutoka nchi wanachama,Manaibu Spika,Wabunge na Mabalozi kutoka nchi wanachama waliopo hapa nchini Tanzania watahudhuria pia.

Aidha, Ndugai amesema wanategemea mkutano huo utaingizia nchi kipato kwa maana ya fedha za kigeni, huku akisema kutakuwa na faida kwa wafanyabiashara wao watakao toa huduma kama vile, wamiliki wa hoteli watakapolala wageni,wauza vyakula yaani wauza migahawa na mahoteli bila kusahau eneo maarufu la forodhani.

Kwa upande wake Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai amesema wageni wanatarajiwa  kuanza kuingia  tarehe  28  agost mpaka tarehe 31 agost.

Mkutano huo wa chama cha mabunge wa chama cha jumuiya ya madola kanda ya afrika ‘’The Commonwealth Pariamentary Association Afrika Region ‘’ hufanyika kila mwaka kwenye nchi wanachama wa chama hicho na kwa mwaka huu mkutano huo utafanyika hapa chini Tanzania, visiwani Zanzibar katika hoteli ya Madinat Al Bahr Kuanzia Agost 31 hadi Tarehe 5,Septemba,2019.

Mwaka jana mkutano huo ulifanyika Gabarone na walishiriki zaidi ya watu mia nne (400),hivyo wanategemea kupata idadi zaidi ya hiyo kwa kuwa waheshimiwa kutoka nchi mbalimbali wameonyesha nia kubwa ya kushiriki 
 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527