POLISI WAZUNGUMZIA TUKIO LA MWANAMKE ALIYEDAIWA KUWA MCHAWI ALIYENASA JUU YA NYUMBA


Mkazi wa Morogoro aliyekutwa akiwa juu ya paa la nyumba huku akiwa amejifunga mavazi ya rangi nyekundu na nyeusi na kuacha kifua wazi eneo la Isele Ilula wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi

JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia na kumhoji mwanamke Kabula Masunga(41), anayedaiwa kufanya ushirikiana baada yakukutwa kwenye paa la nyumba ya Mchungaji Jeremia Charles saa 11 alfajiri juzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Juma Bwire amesema leo Agosti 20,2019 kuwa mwanamke huyo anatuhumiwa kufanya ushirikina huo eneo la Isele Ilula wilayani Kilolo mkoani Iringa na kusababisha taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.

Amefafanua mwanamke huyo ambaye ni mpagani na mkazi wa Morogoro alikutwa akiwa katika mazingira hayo akiwa amejifunga mavazi ya rangi nyekundu na nyeusi lakini kifua aliacha wazi.

"Pia alikutwa akiwa na ungo uliyofungwa kitambaa ya rangi nyeusi na nyekundu.Amekutwa pia na pembe la ng'ombe na alijifunga hirizi mikononi. Mwanamke huyo alikuwa na wenzake wanne inaodaiwa alikuwa anasafiri nao kwa kutumia ungo,"amesema .

Kamanda Bwire amesema kwa sasa wanaendelea kumhoji zaidi ili kufahamu lengo la kufanya ushirikina huo.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527