MKE NA MUME WATUPWA JELA MIAKA 5 KWA KUWAKEKETA WATOTO WAO WATATU


Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela, Thadei Parokwa (43) na mke wake Lowema Thadei (34) kwa kuwakeketa watoto wao watatu. 


Mwendesha mashitaka wa Polisi mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Mkaguzi wa Polisi, Hamilton Moses, alisema shitaka lililowakabili washitakiwa hao kuwa ni ukatili dhidi ya watoto.

Amesema kesi hiyo iliripotiwa kituo cha Polisi Orkesmet tarehe Machi 19, mwaka jana baada ya kukamatwa watuhumiwa hao ambao walidaiwa kuwakeketa watoto hao kwa bibi yao aliyekuwa Kitongoji cha Kangala Kijiji cha Lobosireti Wilayani humo.

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Lugano Kasebele, baada ya kujiridhisha kwa pande hizo mbili, aliwatia hatiani wazazi hao kwenda jela miaka mitano ama faini ya laki sita na fidia ya laki tisa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527