MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU: SINA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR


Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi ya uongozi kwa ngazi ya Urais visiwani Zanzibar.

Makamu wa Rais ameyabainisha hayo Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa sherehe  za kimila ya Wakizimkazi, ambazo hufanyika kila mwaka visiwani humo kwa lengo la kukuza na kudumisha mila na tamaduni za wakazi wake.

''Nataka kusema kwamba kuna maneno maneno kwamba Mama Samia Suluhu anataka kugombea Urais Zanzibar, nataka kuwaambia sio kweli na sina nia hiyo, ukiangalia ngazi ya uongozi ndani ya Tanzania mimi ni namba mbili sina kishawishi chochote kinachonivuta kunileta huku niwe namba tatu sina", amesema Mama Samia.

"Niliona  niliseme hukuhuku lilikotoka kwa sababu maneno yamekuwa mengi, chuki, ufisadi na majungu'', ameongeza.

Hivi karibuni kumekuwa na maneno yanayosambazwa hasa visiwani Zanzibar kuwa Mama Samia ana nia ya kugombea nafasi ya Urais visiwani humo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527