HATIMA YA DHAMANA YA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA KUJULIKANA AGOST 5 | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, August 1, 2019

HATIMA YA DHAMANA YA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA KUJULIKANA AGOST 5

  Malunde       Thursday, August 1, 2019

Mahakama ya Kisutu imekataa na imeutaka upande wa Serikali kuwasilisha kiapo kinzani  kabla ya August 5, 2019 kujibu hoja kuhusu kukamatwa kwa Mwanahabari Erick Kabendera. 


Wakili wake  Shilinde Swedy amewasilisha maombi ya kutaka Kabendera afikishwe Mahakamani kwasababu anashikiliwa  kwa zaidi ya masaa 24 tangu July 29.

Upande wa Jamhuri ulitaka kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani  Agosti 7, mwaka huu, lakni Mahakama ikakataa.

Jamhuri wamekutana na kikwazo hicho leo Alhamisi saa tatu asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile anayesikiliza maombi hayo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai maombi hayo yaliwafikia jana na leo shauri linakuja kwa mara ya kwanza hivyo anaomba apewe muda wa kuwasilisha kiapo cha majibu kinzani Agosti 7 mwaka huu kwa sababu kesho atakuwa Mahakama Kuu katika kesi nyingine.

Wakili wa mwombaji, Shilinde Swedy alidai mteja wake yuko chini ya ulinzi kwa zaidi ya saa 24, hajapata uwakilishi wa aina yoyote hivyo aliomba kesi ije Jumatatu.

Hakimu Rwizile alisema kwa kuwa maombi yamekuja chini ya hati ya dharura, muda ulioombwa na Jamhuri ni mrefu, hivyo maombi hayo yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu.

“Maombi yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu siku ya Jumatatu saa saba mchana, wajibu maombi watajibu wakati wowote kabla ya muda huo,” amesema Hakimu Rwizile.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post