BASATA YAISHANGAA SERIKALI YA KENYA KUUFUNGIA WIMBO WA 'TETEMA' WA RAYVANNY NA DIAMOND PLATNUMZ


Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeshangazwa na Serikali ya Kenya kuuzuia wimbo Tetema wa msanii kutoka Tanzania, Rayvanny aliomshirikisha Diamond Platnumz kupigwa kwenye maeneo ya wazi nchini humo.

BASATA wamesema wimbo huo ni mzuri kwani hauna tatizo lolote na kawaida yao huwa wanakagua nyimbo zote na kama wimbo ukionekana una matatizo huwa wanachukua hatua ikiwemo kuufungia.

“Tumekuwa tukifuatilia nyimbo za wasanii wa hapa nchini na kuwaita wanapokosea. Tunatoa onyo na hata kufungia nyimbo zao, lakini huu (TETEMA) hauna shida ndio maana nasema sijui wametumia vigezo gani kuuzuia usichezwe mchana,” amesema Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza kwenye mahojiano yake na Gazeti Mwananchi.

Wimbo wa Tetema pamoja na Wamlabez wa msanii Sailors wa nchini Kenya zimezuiwa kupigwa maeneo ya wazi nchini Kenya na badala yake zinatakiwa kupigwa katika kumbi za starehe na baa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527