ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MITATU


NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani, linamshikilia Dismas Silyvester (35)  kwa kosa la kumbaka mtoto mdogo mwenye miaka mitatu, huko Mlandizi  A ,kata ya Mlandizi ,Kibaha.


Aidha Mariam Shomari (25) mkazi wa Msongola ,Mlandizi Kibaha ameibiwa mtoto wake mchanga wa miezi mitatu katika mazingira ya kutatanisha ambapo jeshi hilo linaendelea na msako ili kumpata mtoto huyo.


Akithibitisha kutokea kwa tukio la kwanza ,kamanda wa polisi mkoani hapa, Wankyo Nyigesa aliwaambia waandishi wa habari kwamba, Dismas alimuiba mtoto wa miaka mitatu na kwenda nae kichakani na kumfanyia unyama huo.


“Baada ya taarifa kutolewa kwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na raia wema lilimkamata mtuhumiwa na mtoto mchanga huyo katika mashamba ya mbogamboga vichakani “alifafanua Wankyo.


Wankyo alieleza ,uchunguzi unaonyesha mtoto huyo ambae jina limehifadhiwa ,ameingiliwa kimwili.


Akielezea tukio jingine Wankyo alisema, agost 25 saa 7 mchana ,Msongola, Mariam Shomari aligundua kuibiwa mtoto wake mchanga Swaumu Sudi mwenye miezi mitatu.


“Mtoto huyo aliibiwa ndani akiwa chumbani alipokuwa amelala baada ya mama yake kutoka kwenda kuomba kibiriti kwa jirani umbali wa mita 200 na mwanamke ambae hajafahamika hadi sasa”


Inadaiwa mwizi huyo wa mtoto alitumia mbinu ya kuvizia mama wa mtoto kutoka na yeye kufika kwenye nyumba hiyo na kumwambia mtoto mdogo Fatima Sudi miaka mitatu aliyekuwa amebaki na mdogo wake kuwa ametumwa na mama yake kuja kumchukua mtoto huyo ili ampelekee na kufanikisha wizi huo.


Jeshi hilo linaendesha msako mkali wa kumtafuta mwizi wa mtoto ambapo ametoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa ,watendaji wa kata ,wenyeviti wa vitongoji na vijiji pamoja na jamii kutoa taarifa iwao watamtilia shaka mtu ambae anaonekana na mtoto asiye wake.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527