AJALI YA GARI,PIKIPIKI YAUA NA KUJERUHI SHINYANGA MJINI


Gari lenye namba za usajili T 432 ALT Suzuki Vitara limegonga pikipiki na kutumbukia mtaroni na kusababisha kifo cha abiria aliyekuwa amepanda kwenye pikipiki hiyo katika eneo la Ushirika, Shinyanga Mjini barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao ajali hiyo imetokea Agosti 2,2019 majira ya saa mbili na robo usiku ambapo gari ambalo mmiliki wake bado kufahamika likiendeshwa na Salum Saidi (30), mkazi wa Lumumba - Mwanza ambaye ameumia kifua, likitokea Shinyanga kuelekea Mwanza liliacha barabara na kugonga pikipiki yenye namba za usajili T 295 BSG aina ya Kiboko.

"Pikipiki hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Kishimba Sanzago (28) mkazi wa Ibadakuli ambaye ameumia kichwani na kusababisha kifo kwa abiria wa pikipiki hiyo ambaye hajafahamika jina, kabila wala makazi yake umri kati ya miaka 35-40",ameseama

"Majeruhi wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo",ameongeza Kamanda Abwao.

Aidha amekitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni ulevi kwa dereva wa gari na amekamatwa na vyombo husika vipo kituoni.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527