WATOROSHAJI DHAHABU KATAVI KUKIONA


Mkuu wa mkoa wa Katavi  Juma Homera ameapa kupambana na wanaotorosha dhahabu huku mpaka sasa watu wawili wakishikiliwa na jeshi la polisi kwa kununua dhahabu kinyume cha sheria mkoani humo.

RC Homera akiwa ziarani katika migodi mbalimbali ikiwemo Dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi mining  alieleza anachotaka wachimbaji wadogo wakauuze madini yao katika soko la madini la mkoa huo.

Homera alianza majukumu ya ukuu wa mkoa ikiwa soko limeshafanya biashara kwa kununua dhahabu gram 238, May 23/2019 jambo ambalo lilimfanya aanze kufatilia na kubaini dhahabu nyingi inayopatikana Mkoani Katavi inauzwa nje ya mkoa wa  Katavi nakupelekea soko hilo kusua sua.

Kufuatia jambo hilo limemfanya  Homera kuyafanyia kazi mapungufu ya soko hilo, mpaka sasa ununuzi na uuzaji wa madini ni Grams 6317.2 sawa na Kg 6 na Grams 317.2 yenye thamani ya Tshs.Million 519,155,127.56 zimenunuliwa kwa kipindi cha Mei na June 30/2019 na serikali kupata mrahaba (Royality7%) Tsh Milioni 36,340,858.92 na Service levy  0.3% Tsh.milioni 1,401,718.85.

Aidha ameimarisha mifumo ya Benk mbili katika soko hilo na ameendelea kuwa bana mablokers na wanunuzi wenye leseni na wachimbaji mbalimbali  kuhakikisha pia wanauza madini yao kwenye soko la mkoa ili tujenge uchumi wa Tanzania na kumuunga mkono Rais wetu Dkt.John Joseph Pombe Magufuli katika kuinua uchumi na miundombinu ya nchi hii kwa kulipa kodi


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527