UVCCM TAIFA YAFANYA MAFUNZO MAALUM KWA WASICHANA MKOA WA DAR ES SALAAM


Makamo wa  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Vijana wa CCM Taifa Ndg Tabia Mwita amefungua mafunzo  Maalum kwa Wasichana kwa Mkoa wa Dar es Salaam.


Mafunzo hayo Yaliyosimamiwa na kuratibiwa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Rose Robert Manumba kwa Kushirikiana Taasisi ya Kijerumani FES kwa lengo la kuwaelimisha na kuwaongezea ujuzi na Maarifa yakiuongozi.

Pamoja na kufungua Mafunzo hayo Miongoni mwa waliyotoa na mada ni Ndg.Tabia Mwita na  amewasilisha Mada ya Ushiriki wa wanawake katika siasa ambavyo amesisitiza wanawake kuendelea kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa bila kuogopa. Amewasihi wanawake kujiamini na kutokukubali kukatishwa tamaa.

Makamu huyo  amesisitiza umuhimu wa kuwa na umoja na mshikamano ili kuendeleza kusaidia Serikali katika juhudi zinazofanyika kumuinua Mwanamke.

Aidha, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa Rose Manumba akiwa  amesisitiza kuwa ni muhimu sisi kama wasichana kuwa sehemu ya mabadiliko tunayotamani kuyaona katika nchi yetu na hata duniani kwa ujumla. Tuwe  tayari kutumikia nafasi zetu popote pale tulipo kuendelea kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dr. John Pombe Magufuli anayepambana usiku na mchana kumuinua mwanamke wa kitanzania ili kuleta maendeleo katika Taifa letu.

Wameshiriki wakufunzi mbalimbali kama Dorris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation aliyewasilisha mada ya Mchango wa asasi za kiraia katika kumuinua Mwanamke na Suma Mwaitenda ambaye ni Mkurugenzi wa FURSA, kutokea Clouds Media Digital aliyewasilisha mada ya;  Namna gani msichana anaweza kuziona na kuzipata Fursa.

 Ndg. Japhary Kubecha ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya UVCCM Taifa katika kufunga mafunzo hayo amesisitiza wanawake kujituma katika kazi na sio kuridhika na nafasi mbalimbali ambazo wanaweza kupata kwa kigezo kuwa ni wanawake.

Mafunzo haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali; Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni Lilian Rwebangira, Abdul-Rahman Killo na Mwanaidi ambao ni Maafisa kutoka UVCCM Makao Makuu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527