TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI

Frank Lampard amepigwa picha katika uwanja wa Stamford Bridge anapokaribia kuwa kocha mpya wa Chelsea. (Mail)
Kuidhinishwa kwa Lampard kuwa kocha mpya wa Chelsea kulicheleweshwa Jumatano jioni baada ya mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram kukumbwa na changamoto za kiufundi hali ambayo ilifanya kuwa vigumu kuchapisha picha au kuweka video mtandaoni. 

Klabu hiyo ilitaka mitandao hiyo ya kijamii kurejea katika hali yake ya kawaida kabla ya kufanya tangazo hilo. (Mirror)

Chelsea pia imeanza mazungumzo ya kandarasi mpya ya na kiungo wa kati wa miaka 20 Mason Mount, amabaye aliichezea Derby msimu uliopita chini ya ukufunzi wa Lampard. (Evening Standard)

Manchester United wanataka kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24 kutoka Sporting Lisbon. (Sky Sports)Bruno Fernandes

Tottenham imesitisha mazungumzo yake na Real Betis kumhusu kiungo ya kati wa Argentina Giovani Lo Celso, 24, baada ya vilabu kushindwa kuafikiana malipo. (Sky Sports)

Arsenal wamepewa nafasi ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Mbrazil Malcom, 22, lakini azma yao kubwa ni kumnasa mshambuliaji wa Ivory Cost wa miaka 26, Wilfred Zaha kutoka Crystal Palace. (Mirror)

Gunners wana pauni milioni 70 wanapojianda kuweka dau la pili la kumnunua Zaha, japo kuwa Palace wanamini thamani ya mshambuliji huyo ni pauni milioni 80(Sky Sports)Zaha aliifungia Palace mabao 10 katika msimu wa 2018-19

Manchester City huenda wakamsaini mlinzi wa Uholanzi wa miaka 24 Nathan Ake kutoka Bournemouth msimu huu. (L'Equipe - in French)

Tottenham wanamtaka mashambulizi wa roma na timu ya taifa ya Italia Nicolo Zaniolo, 22, na wako tayari kumuuza mlinzi wa Ubeliji Toby Alderweireld, 30, ili wapate fedha za kugharamia mkataba huo. (Mail)

Agenti wa Romelu Lukaku amaefanya mazungumza mapya na Inter Milan lakini klabu hiyo ya Italia bado inashauriana na Manchester United kuhusu ada ya kiungo huyo wa Ubelgiji aliye na miaka 26. (Sky Sport Italia - in Italian)Romelu Lukaku

Bayern Munich wameipiku Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumsaini beki mkabaji wa Ureno Joao Cancelo,25, kutoka Juventus. (Corriere dello Sport via Manchester Evening News)

Everton wamepokea maombi kutoka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Ujerumani maarufu Bundesliga na hampionship ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa miaka 22, Joe Williams. ((Liverpool Echo))

Southampton hawana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Ureno Andre Silva, 23, kutoka AC Milan licha ya tetesi kutoka Italia kuashiria vingine. (Daily Echo)
Tottenham huenda ikawauza beki wa England Kieran Trippier, 28, na Danny Rose, 29, wanapojianda kutoa maombi ya kumnunua mlizi wa Fulham muingereza Ryan Sessegnon, 19.(Mirror)

Newcastle imewasiliana na kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez okuhusu uwezekano wake kuchukua nafasi ilioachwa wazi na Rafael Benitez kama meneja wao mpyaa. (Sun)

CHANZO.BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post