TAMASHA LA ZIFF 2019 LATOA MAFUNZO KWA WATOTO MFANANO (DOWN SYDROME) | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 10, 2019

TAMASHA LA ZIFF 2019 LATOA MAFUNZO KWA WATOTO MFANANO (DOWN SYDROME)

  Malunde       Wednesday, July 10, 2019
Na Andrew Chale, Zanzibar

TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) la 22 kwa mwaka huu leo limeendesha mafunzo kwa Watoto wenye tatizo la Down Syndrome ama Watoto mfanano kama wanavyojulikana visiwani Zanzibar.

Mafunzo hayo yanayotolewa na ZIFF kwa kushirikiana na taasisi ya kutoka Uholanzi ya Media Lab ambayo imekuwa ikitoa mafunzo kwa watoto mbalimbali visiwnai hapa kwa kutumia teknolojia kwa masuala ya sanaa ikiwemo utengenezaji wa vikatuni, Uigizaji, utangazaji, uandishi wa habari, kuchora na mambo mengine katika masuala ya Sanaa.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Warsha za ZIFF 2019, Ahmed Harith amebainisha kuwa, mafunzo hayo ni ya mara ya kwanza kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ambapo wanatarajia Watoto zaidi ya 1,000 kushiriki mafunzo hayo.

“Mafunzo haya yanatolewa kila siku kuanzia Julai 5 na yataisha mpaka mwisho wa tamasha. Ambapo kwa siku watoto zaidi ya 100 wanapata kushiriki.Watoto hao wanatoka shule mbalimbali za visiwani hapa na baadhi yao nje ya skuli” alisema Ahmed Harith.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Down syndrome Initiative Zanzibar, Bi. Ahlam Abdalla Azzam amelipongeza tamasha la ZIFF 2019 kwa kuwakumbuka watoto hao ambao wameweza kujifunza mambo mbalimbali kama watoto wengine licha ya uelewa wao kuwa mdogo.

“Tunaipongeza ZIFF kwa kuwajali watoto Mfanano wameweza kujifunza vitu vingi ikiwemo kuimba, kucheza na kufanya vitu vya ubunifu.Pia wameweza kujfunza namna ya kuchora michoro na na kutengeneza vikatuni kupitia program za kisasa za teknolojia ya Media Lab” alieleza Bi. Ahlam Abdalla Azzam.

Zanzibar inaelezwa kuwa na Watoto wengi wenye tatizo la Down Syndrome ambapo Serikali na wadau wamekuwa wakichukua hatua za kuwasaidia watoto hao. 

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post