MUME AMTAFUNA MKEWE MDOMO NA SIKIO | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, July 20, 2019

MUME AMTAFUNA MKEWE MDOMO NA SIKIO

  Malunde       Saturday, July 20, 2019
Mwanamke wa miaka 39 mkaazi wa Tanga Kona, Kenya anauguza majeraha baaada ya mume wake kumnyofoa mdomo na sikio kufuatia ugomvi baina yao.

Jackline Kerubo, mama wa watoto sita, alisema alitaka kwenda kuchuma mboga katika shamba la jirani yake lakini mume wake alimkataza.

Kerubo ambaye ni mume wake aliyefunga naye ndoa miaka 21 iliyopita, anasema kwa sasa anahofia maisha yake pamoja na watoto wake.

Alisema jirani yake aliingilia kati baada ya mume wake kuapa kumpa fundisho . Hata hivyo baada ya kipigo hicho Mume wake alitoweka nyumbani.

Akizungumza na waandishi wa habari, alisema mume wake alitenda unyama huo akiwa jikoni kwa kumpiga kichwani na baadae kumtafuna mdomo na sikio.

Mkuu wa Polisi Maryline Oundo aliwaomba wanandoa kutafuta ushauri wanapokuwa na mizozo na kuitaka jamii kutoa taarifa za kesi zinazokiuka haki za binadamu ili kupata msaada sambamba na watuhumiwa kuchukuliwa hatua.

Bi Kerubo kwa sasa anapatiwa hifadhi katika kituo cha polisi Nambale wakati maafisa polisi tayari wameanza kazi ya kumtafuta mtuhumiwa.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post