STAND UNITED WAANZA HARAKATI KUREJEA LIGI KUUWadau wa Soka mkoani Shinyanga wanatarajia kufanya mkutano siku ya Jumapili Julai 14,2019 kwa ajili kujadiliana na kutafakari kwa pamoja namna gani wajipange kuhakikisha wanairudisha timu ya Stand United 'Chama la Wana' kwenye Ligi Kuu Msimu wa 2020/2021.


Mkutano huo utafanyika siku ya Jumapili katika Uwanja wa CCM Kambarage kuanzia saa 9 kamili alasiri hadi saa 12 jioni.

Mwenyekiti wa Stand United Dkt. Ellyson Maeja amesema mkutano huo unaoongozwa na Kauli mbiu 'Kwa Pamoja Tunaweza' utahudhuriwa na wanachama,wapenzi na wadau wa Stand United.

"Mkutano utaongozwa na mada 'Kukaa pamoja na kutafakari ni kwa namna gani kwa 'Umoja Wetu Sisi Sote'  tukijipanga na kushirikiana kwa moyo wa dhati kwa Pamoja Tunaweza kurudisha timu yetu pendwa Ligi kuu Msimu wa 2020/2021",amesema Dkt. Maeja.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post