RC SIMIYU APOKEA MSAADA WA BAISKELI ZA WALEMAVU 48

Mmoja wa watoto wenye ulemavu akisaidiwa kuwekwa kwenye moja ya baiskeli 48 zilizotolewa kwa pamoja kati ya kampuni ya Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) na taasisi ya Wheelchair Foundation ya Marekani zenye thamani ya Sh 20 milioni katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu. 
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa baiskeli 48 za watu wenye ulemavu  zilizotolewa kwa pamoja kati ya kampuni ya Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) na taasisi ya Wheelchair Foundation ya Marekani zenye thamani ya Sh 20 milioni katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu. 


Mkurugenzi wa taasisi Wheelchair Foundation,Charli Butterfield akimpa zawadi mmoja wa washindi wa mashindano ya baiskeli kwa watu wenye ulemavu katika kusherekea Jambo Festival kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu.



 Mkurugenzi wa kampuni ya kitalii ya Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL)akimpa zawadi mmoja wa washindi wa mashindano ya baiskeli kwa watu wenye ulemavu katika kusherekea Jambo Festival kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu.



Ngoma za utamaduni wa jamii ya wasukuma huwa ni moja ya kivutio kikubwa wakati wa sherehe za kila mwaka zaJambo Festival wilayani Bariadi.


Katibu Tawala mkoa wa Simiyu,Jumanne Sagini(kulia) akiwaongoza viongozi kuondoka mara baada ya sherehe zilizoambana na zawadi mbalimbali kwa washiriki kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi.



Mwandishi Wetu,Bariadi 
Watu wenye ulemavu wa miguu mkoani Simiyu wamenufaika kwa kupata msaada wa baiskeli zitakazowawezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine  bila vikwazo baada ya shirika la Wheelchair Foundation  la nchini  Marekani na Friedkin Conservation Fund (FCF) kutoa baiskeli 48 zenye thamani ya Sh 20 milioni.

Mkurugenzi  wa taasisi ya Wheelchair  Foundation ,Charli Butterfield alimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka baiskeli hizo alisema zitawasaidia watu wenye ulemavu kujishughulisha na shughuli za maendeleo na kuona wapo watu wanaowajali katika hali waliyonayo.

Alisema taasisi hiyo imekua ikiwajali watu wenye uhitaji wa baiskeli duniani kote kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita na hapa nchini wameshatoa jumla ya baiskeli 2,240 katika mikoa tofauti na wataendelea kufanya hivyo kadiri wasamaria wema wanavyochangia taasisi yao.

Akipokea baiskeli hizo Mkuu wa mkoa huo alisema ni muhimu sana kuwepo na ushirikiano wa kuwafikia wenye ulemavu ambao hawawezi kumudu gharama za kununua baiskeli hizo na kuiomba taasisi hiyo iendelee kusaidia zaidi katika eneo la kuwawezesha watu wenye ulemavu na sekta ya afya na elimu.

Aliongeza kuwa  wakati wote serikali ya mkoa inatambua ushirikiano wa muda  mrefu uliopo kati ya nchi mbili za Marekani na Tanzania na mkoa utaendeleza mahusiano hayo kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili katika kuhamasisha maendeleo ya mshikamano.







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527