SANAMU YA MWALIMU NYERERE BURIGI- CHATO YAZUA GUMZO MTANDAONI

Jana Julai 9, 2019 kulikuwa na hafla ya uzinduzi wa Hifadhi mpya ya wanyamapori ya Burigi-Chato, Hafla ambayo ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumkabidhi Sanamu hiyo ya Baba wa Taifa. 

Rais Dkt. Magufuli alitoa maelekezo kuwa Sanamu hiyo aliyokabidhiwa ijengewe eneo zuri katika hifadhi hiyo ya Burigi Chato ili watalii wakija waweze kumjua zaidi Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwenye uzinduzi huo, Rais Magufuli alikabidhiwa sanamu ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla yenye ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya wanyama pori.

Muonekano wa sanamu hiyo, umezua mijadala tofauti tofauti kwenye mitandao ya kijamii wengi wakionekana kushangazwa na muonekano wake wakidai kuwa hauendani hata kidogo na sura ya Mwalimu Nyerere.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527