NHIF TANGA YAOKOA MILIONI 65.1 AMBAZO ZINGEWEZA KUHUJUMIWA NA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA

 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza leo wakati akifungua kikao kazi cha Waratibu wa Bima ya Afya kilichowahusisha waratibu kutoka wilaya zote za mkoa huu kilichofanyika wilayani Korogwe.


 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza leo wakati akifungua kikao kazi cha Waratibu wa Bima ya Afya kilichowahusisha waratibu kutoka wilaya zote za mkoa huu kilichofanyika wilayani Korogwe.
 MSIMAMIZI wa Ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo akiwasilisha mada ya madai kwenye kikao hicho
 Afisa udhibiti ubora Dkt Mussa Sendama akiwasilia mada kwenye kikao hicho
 AFISA Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemence akieleza mada kuhusiana na uanachama na vitambulisho
 Mhasibu wa NHIF mkoa wa Tanga Vistus Tulusasila  akieleza jambo kwenye kikao hicho
 MRATIBU wa Bima ya Afya Jiji la Tanga Dkt Jestina Msumaria akijitambulisha kwenye kikao hicho
Mmoja wa washiriki kwenye kikao hicho akijitambulisha

 MRATIBU wa NHIF wilaya ya Kilindi mkoani Tanga Omari Javu akijitambulisha

 Sehemu ya waratibu wa Bima ya Afya kutoka wilaya mbalimbali wakifuatilia mada mbalimbali kwenye kikao hicho
 Sehemu ya waratibu wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga wakichukua dondoo kwenye kikao hicho

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi hicho



MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umefanikiwa kuokoa kiasi cha sh.milioni 65,155,468 ambazo zingeweza kuhujumiwa na vituo vya kutolea huduma kwenye mwaka huu kutokana na madai ya kughushi. 

Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati akifungua kikao kazi cha waratibu wa Bima mkoa huo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani Korogwe. 

Alisema kwenye mwaka wa fedha 2018/2019 walifanya juhudi kubwa katika kuokoa fedha hizo ambazo zingeweza kuhujumiwa na vituo kutokana na madai ya kughushi ambayo vituo vilitaka kufanya wamezuia kutokana na kufanya ukaguzi makini. 

Alisema vituo ambavyo vilifanyiwa ukaguzi ni 28 kati ya hivyo 20 ni vya serikali na 8 ni dini na binafasi huku akisisitiza umuhimu wa vituo kufuata miongozo na taratibu zilizowekwa za tiba la sivyo hatua zitachu kuliwa na sheria ambazo zinaweza kuwaletea matatizo kwenye vituo au wahusika wenyewe kushtakiwa. 

Meneja huyo alisema mfuko huo umefanya juhudu kubwa kwa kushirikiana na wadau wengine kwenye vituo vinavyotoa huduma ambapo kwa mwaka 2018/2019 mfuko huo umelipa vituo vya serikali bilioni 3.7 sawa na ongezeko la milioni 427.7 asilimia 11 hivyo kuna maendeleo makubwa huku akieleza kwamba huduma zinazidi kuboreka mkoani Tanga. 

Alisema pia kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wamelipa kiasi cha Bilioni 3.6 katika mwaka wa fedha 2018/2919 hiyo ukilinaganisha mwaka wa fedha 2017 /2018 ilikuwa ni Bilioni 2.6 hilo ni ongezeko la Bilioni 1.1 ongezeko la asilimia 39 

“Kupitia matokeo haya bima ya Afya ina haja ya kutembea kifua mbele wakiwemo watoa huduma lakini nivitake vituo vinavyohujumu na vilihudumu viache mara moja kwani mwaka huu wa fedha tumejipanga vilivyo na tutakwenda kila kituo kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa”Alisema Meneja huyo. 

Awali akizungumza wakati akiwasilisha mada ya majukumu ya waratibu wa mfuko huo,Afisa udhibiti ubora Dkt Mussa Sendama alisema lazima watambue makundi yenye uhitaji kwani hiyo itasaidia kuwezesha mfuko huo kusonga mbele. 

“Tutumie nafasi zetu tuweze kuwasaidia ongezeko la wananchi wenye uhitaji kwenye makundi mbalimbali ikiwemo kushauri kueleza jamii masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya”Alisema. 

Hata hivyo alisema kwamba suala lingine ni kwenye maeneo yao waweze kuwashawishi watu waweze kujiunga na mfuko ili kuweza kuboresha mafanikio. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527