AUA MTU MMOJA,AJERUHI WAWILI KWA MSHALE BAADA YA KUNYIMWA BIA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 30, 2019

AUA MTU MMOJA,AJERUHI WAWILI KWA MSHALE BAADA YA KUNYIMWA BIA

  Malunde       Tuesday, July 30, 2019
Kijana mmoja ambaye jina lake halijajulikana ameibua taharuki katika Kijiji cha Kwitete Wilaya ya Serengeti mkoani Mara nchini Tanzania baada ya kutuhumiwa kuua mtu mmoja na kujeruhi wawili akiwemo baba yake wa kambo kwa sababu ya kunyimwa bia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki jana Jumatatu Julai 29, 2019 alithibitisha kuwa tukio hilo limetokea Jumapili Julai 28, 2019 kijijini hapo na mtuhumiwa amekimbia wanaendelea kumsaka.

Amesema aliyefariki ni mgeni hajatambulika jina, lakini kabila lake ni Msukuma ambaye aliongozana na mtu mwingine kwenda kwenye mji huo kwa ajili ya kumsalimia mama mwenye mji ambaye pia ametoroka na kijana wake.

Ndaki amesema walinunua kreti ya bia wakati wanakunywa, mtuhumiwa alipewa chupa mbili alipotaka tena wakamnyima ndipo akaingia ndani na kutoka na upinde na kuanza kuwashambulia na kusababisha mauaji ya mtu mmoja na kujeruhi wawili.

Mmoja wa wahudumu wa Hospitali Teule ya Nyerere ambaye hakutaka kutaja jina lake, amethibitisha kupokea mwili wa mtu anayedaiwa kupigwa mshale ambao umeletwa na polisi wa wilaya ya Serengeti na uchunguzi utafanyika baada ya ndugu kujitokeza.


Na Anthony Mayunga - Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post