MAKONDA APOKEA MIL 23 KUFADHILI MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO 60 WENYE UHITAJI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 25, 2019

MAKONDA APOKEA MIL 23 KUFADHILI MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO 60 WENYE UHITAJI

  Malunde       Thursday, July 25, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 25 amepokea zaidi ya Shilingi Milioni 23 kutoka kwa wadau ambao wameguswa na kampeni aliyoanzisha ya ufadhili wa matibabu ya upasuaji moyo kwa watoto 60 kutoka familia zenye hali duni.


Miongoni mwa Wadau waliomuunga Mkono  Makonda ni Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe. Sylvester Koka ambaye amekabidhi hundi ya Shilingi milioni 10 kwa ajili ya matibabu ya watoto 5 huku Mkurugenzi wa Dorka Catering Bi. Dorothy Kansolele akichangia milioni 6 na  mkurugenzi wa kampuni ya Abe Professional Sound Bw. Abraham Ngomko akichangia Milioni 6 kwaajili ya matibabu ya watoto 3.

Akipokea fedha hizo Makonda amezikabidhi kwa uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kueleza kuwa zitasaidia kugharamia zaidi ya Watoto10 kwenye upasuaji wa awamu ya pili.

Aidha Makonda amewashukuru wadau wote wanaondelea kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo inayolenga kuokoa maisha ya watoto ambao wangeweza kupoteza maisha kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Kwa upande wao wadau waliokabidhi fedha hizo wameeleza kuwa wataendelea kuunga mkono zoezi hilo kwa kuongeza fedha nyingine kwakuwa wanaamini kampeni aliyoanzisha Makonda ni njema na linapaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali ili kuokoa maisha ya watoto.

Itakumbukwa kuwa Makonda alitoa ahadi ya kufadhili matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto 60 kwa muda wa miezi sita ambapo kila mwezi watatibiwa watoto10 na hadi sasa tayari amefanikisha matibabu ya watoto 30 kati ya 60 alioahidi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post