MAJAMBAZI WAJIFANYA TRAFIKI NA KUTAPELI MADEREVA WA MAGARI

Baadhi ya madereva wanaoendesha magari yanayokwenda nchi mbalimbali kupitia Tanzania (IT) wameibua madai ya watu wanaojifanya askari wa usalama barabara na kuwadai fedha.

Takribani wiki mbili zilizopita madereva hao wamedai wenzao watano wamekumbana na matrafiki hao feki maeneo ya Kimara na Mbezi jijini Dar es Salaam wakati akitokea Bandari ya Dar es Salaam kupeleka magari katika nchi hizo.

Alipoulizwa na Mwananchi juzi Ijumaa Julai 12, 2019 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hawajapata taarifa za uwepo wa matukio hayo, kuahidi kufuatilia.

Kwa mujibu wa maelezo ya madereva hao, askari hao feki hutumia foleni katika maeneo hayo kuwasimamisha na kuibua makosa mbalimbali na kudai fedha ili kuwaachia.

“Wametengeneza vitambulisho kujitambulisha kama maofisa wa polisi na huvaa nguo za kiraia. Mara nyingi huwatajia madereva kosa la kutosimama kwenye alama za kuvuka watembea kwa miguu,” amesema Dumisani Mpofu.

Mpofu amesema aliporwa na watu hao Dola 300 za Marekani na fedha ya Tanzania.

Amesema watu wanne walifika kwenye gari lake akiwa katika foleni eneo la Kimara, kutoa kitambulisho wakidai ni askari na kumtaka ashuke kwenye gari.

“Niliteremka kwenye gari kama walivyoagiza kwa kuwa walitoa kitambulisho, sikuwatilia shaka kwa kuwa ilikuwa saa mbili usiku.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post