KIJANA AMLAWITI MAMA YAKE MZAZI...TAYARI KADAKWA NA POLISI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 4, 2019

KIJANA AMLAWITI MAMA YAKE MZAZI...TAYARI KADAKWA NA POLISI

  Malunde       Thursday, July 4, 2019

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Mazengo Chati kwa kumlawiti mama yake mzazi akiwa hajitambui, katika Kijiji cha Manchali wilayani Chamwino, jambo ambalo ni kinyume kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Kamanda Muroto ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alieleza kijana Mazengo Chati mwenye umri wa miaka 28, amembaka mama yake mzazi mwenye miaka 56 na ametenda kosa hilo kwa madai ya ulevi pamoja na imani za kishirikina.

Kamanda Muroto amesema kuwa "tukio la kijana Mazengo limetokea katika Kijiji cha Manchali ambapo kijana huyo alimlawiti mama yake mzazi akiwa hajitambui, na kwa sasa tunamshikilia kwa ajili ya kumfikisha mahakamani"

Aidha Kamanda huyo amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wengine wawili, kwa makosa ya ulawiti na ubakaji wa watoto na wazee huku mtuhumiwa mmoja akiuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kukutwa akiwa anambaka mwanafunzi wa miaka nane.
Chanzo - EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post