IGP SIRRO ATOA ONYO KWA ASKARI WALA RUSHWA


Mkuu  wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amewataka askari wote kuzingatia nidhamu na kujiepusha na vitendo vya rushwa katika utendaji wao wa kazi na kwamba watakaoshindwa kufuata misingi hiyo, hawatakuwa na nafasi.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Musoma, wakati akifanya ukaguzi wa majengo mapya ya ghorofa ya nyumba za askari.

IGP Sirro alisema wapo askari ambao bado hawataki kuzingatia taratibu za kinidhamu zinazotakiwa na kamwe hawezi kuwavumilia kama hawataweza kubadilika.

Alisema nidhamu ndiyo jambo la msingi kwa askari popote alipo na anapokuwa akitekeleza majukumu yake ya kila siku.

IGP Sirro alisema licha ya nidhamu lipo suala la rushwa ambalo pia limekuwa likimchukiza na kuwataka askari kujiepusha na masuala ya kuomba na kupokea rushwa.

Alisema bado wapo askari ambao hawataki kubadilika na kuachana na vitendo vya rushwa na kudai kamwe hawatakuwa na nafasi ya kulitumikia jeshi hilo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post