WIKI YA UTUMISHI WA UMMA : WAFANYAKAZI PSSSF WAWATEMBELEA WASTAAFU KUHAKIKI TAARIFA ZAO


Afisa Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Asmahan Haji, (waliyevaa hijab), akizungumza na baadhi ya wastaafu ambao ni wanachama wa PSSSF kwenye kituo cha Shirika la watawa wa mabinti wa maria Kipalapala, Mkoani Tabora Juni 19, 2019.
Mmoja wa wanachama wa PSSSF, (kushoto), akizungumza na ujumbe wa wafanyakazi wa PSSSF ukiongozwa na Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tabora, Bw. Jacob Cornel Sulle (wapili kulia), Afisa Hudma kwa Wateja, Bi. Asmahan Haji (watatu kulia) na Afisa Malipo, Bw. Felichism Mtenga (wa kwanza kulia).
Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tabora, Bw. Jacob Cornel Sulle akizungumza na wazee hao.
Afisa Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Asmahan Haji, (waliyevaa hijab), akizungumza na baadhi ya wastaafu ambao ni wanachama wa PSSSF kwenye kituo cha Shirika la watawa wa mabinti wa maria Kipalapala, Mkoani Tabora Juni 19, 2019.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bi. Vupe Ligate, (kulia), akimsikiliza mwanachama huyu wa PSSSF ofisini kwake jijini Dodoma Juni 19, 2019.
Mwanachama huyu wa PSSSF (kulia), akitoa maoni yake mbele ya mfanyakazi wa Mfuko huo makao Makuu Dodoma Juni 19, 2019.
Baada ya kuwahudumia wanachama hawa wa PSSSF kwenye ofisi za makao makuu Dodoma, uliwadia wakati wa kuwa na kumbukumbu ya picha ya pamoja na viongozi wa Mfuko.
NA K-VIS BLOG, TABORA NA DODOMA
MOJA ya matukio yaliyoorodheshwa kwenye kalenda ya umoja wa Afrika (AU) yanayopaswa kutekelezwa na nchi wanachama wa umoja huo kila mwaka ni pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma.

Hapa nchini siku ya utumisji wa Umma huadhimishwa kila mwaka na mwaka huu tayari imeanza tangu Juni 16 na kilele chake ni Juni 22, 2019, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi.”

MFUKO mpya wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo zimeshiriki kwa vitendo katika shughuli mbalimbali zinazohusu utumishi wa umma ambako huko Tabora, watumishi wa PSSSF walitoka ofisini na kwenda kwenye Shirika la watawa wa mabinti wa Maria Kipalapala, kiasi cha kilomita 10 kutoka Tabora mjini ili kuwahakiki wastaafu wa Mfuko huo.

Watawa hao ambao baadhi yao ni wazee, walikuwa watumishi wa umma katika sekta za elimu (walimu), na seka ya afya (manesi) na kutokana na umri wa mkubwa wengine hawaweze kutok kufuata huduma nje ya makazi yao, anasema Meenja wa PSSSF mkoa wa Tabora, Bw. Jacob Cornel Sulle.

Meneja huyo anasimulia, “Tumekuja hapa kuwatembelea wanachama wetu kwa nia ya kuwahudumia, kuna wastaafu ni wazee hawawezi kufika ofisini kwentu ili kuhakiki taarifa zao, hivyo tumefika hapa ili tujiridhishe kwa kuwaona physically.” Alisema Meneja wa PSSSF Mkoa wa Tabora, Bw. Jacob Cornel Sulle.

Aidha wafanyakazi wa PSSSF kutoka Makao Makuu ya Mfuko huo jijini Dodoma walishiriki kikamilifu katika kuhudumia wanachama wake kwa kusikiliza maoni yao kwa lengo la kubaini maeneo yenye kasoro ili kuboresha huduma kwa lengo la kutoa huduma bora “PSSSF ni mfuko mpya, hivyo kwa mwaka huu katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma, wakurugenzi wote wakiongozwa na viongozi wa Mfuko watawasikiliza wanachama kwa lengo la kubaini maeneo yanayohitaji kuboreshwa kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wanachama wetu”, alisema Kaimu Mkurugenzi Mkuu.

 Bi.Vupe Ligate Bi. Ligate alisema, Mameneja katika ofisi zote pia watasikiliza wanachama kwa lengo la kuboresha huduma. PSSSF ilianza kufanya kazi Agosti 1, 2018. Mfuko una ofisi Tanzania Bara pamoja na Tanzania visiwani. Siku zote lengo la Mfuko ni kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wanachama wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527