MATOKEO MICHEZO YA UMITASHUMTA 2019: MIKOA 12 IMEFUZU FAINALI MBIO ZA MITA 1500


Mwanariadha kutoka mkoa wa Arusha Damian Christian akiwaongoza wenzake katika mbio za mita 1500 hatua ya nusu fainali leo.
Washiriki wa mbio za kupokezana vijiti kutoka mikoa mbalimbali wakishiriki mbio za mita 400 leo.

Na Mathew Kwembe, Mtwara
Jumla ya washiriki 30 kutoka mikoa 12 nchini wamefuzu hatua ya fainali kushiriki mbio za mita 1500 zilizopangwa kufanyika kesho katika uwanja wa chuo cha ualimu Mtwara.

Washiriki hao 15 wavulana na 15 wasichana watashindana katika fainali za mbio ndefu za mita 1500 kwa ajili ya kuwapata washindi watatu kwa upande wa wavulana na washindi watatu kwa wasichana ambao wataibuka na medali za dhahabu, fedha na shaba.

Kwa mujibu wa Mratibu wa mashindano ya UMITASHUMTA taifa bwana Leonard Thadeo, mchezo huo wa riadha utachezwa kesho asubuhi ambapo utatanguliwa na fainali maalum za mbio fupi za mita 100 kwa wavulana na wasichana na kufuatiwa na mbio fupi za mita 200 kwa wavulana na wasichana.

Bwana Thadeo amewataja waliofuzu fainali za mbio mita 1500 ni pamoja na Damian Christian wa Arusha, Hoja Samwel wa Simiyu, Robert Franciswa Singida, Frank Mashaka wa Mwanza, Paschal Juma wa Tabora na Jackson Renatus wa Geita.

Wengine Amiri shaban wa Singida, Emanuel Ernest wa Manyara, Azari philipo wa Kigoma, Tululi Masanja wa Morogoro, Masanja Ngado wa Tabora, David Paulo wa Mara, Lenard Juma wa Geita, Saimon sangalali wa Mara na Maraba Madoshi wa Mwanza.

Kwa upande wa wasichana waliofuzu mita 1500 ni pamoja na Nyanzabe Mhalu wa Mara, Agnes Joseph wa Tabora, Salma Charles wa Shinyanga, Valaria wa Singida, Salma Musa Ismail wa Mwanza, na Faidha Ally wa Singida.

Washiriki wengine ni Grace Mpina wa Geita, Salome Ngogene wa Iringa, Taus Saimon wa Tabora, Hasja Mwinga wa Mbeya, Modesta Juma wa Geita, Winfrida Marwa wa Mara, Anita Fred wa Songwe na Veronica Lubora wa Songwe.

Wakati huo huo michezo mbalimbali imeendelea leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara ambapo katika matokeo ya mpira wa mikono kwa wavulana Tabora iliifunga Mtwara 13-05, Lindi waliwafunga Pwani 05-03, shinyanga wasichana waliwafunga Rukwa 09-05, Kigoma wasichana walifungwa na shinyanga 07-10, na Njombe wavulana walifungwa na Lindi 09-12.

Matokeo mengine yanaonyesha Mwanza wasichana walifungwa na Mbeya 10-12, katavi wavulana walifungwa na Dodoma 10-19, Manyara wasichana waliwafunga Kagera 18-4, huku Simiyu wavulana wakiwafunga Songwe 11-06, Dodoma wasichana wametoka sare na Dar es salaam kwa 17-17, na Mwanza wavulana wamewafunga Manyara kwa 18-16.

Pia Mtwara wasichana imefungwa na Geita kwa 03-22, Arusha wavulana wamefungwa na Morogoro 10-35, Simiyu wasichana wamefungwa na Katavi kwa 03-06, Dar es salaam wavulana wamewafunga Singida kwa 27-13, Singida wasichana wamewafunga songwe kwa 08-05 na Pwani wavulana wamewafunga Kigoma kwa magoli 12-08, Songwe wavulana wamefungwa na Geita kwa 14-22, Mara wasichana wamewafunga Rukwa kwa 19-03, Mara wavulana wamewafunga Iringa 38-06, Geita wasichana wamewafunga Morogoro 13-11 na Mtwara wamefungwa na Tanga kwa 06-18

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527