Picha : MASHINDANO YA UMITASHUMTA 2019 SHINYANGA YAFUNGWA

Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela amefunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA – 2019) mkoa wa Shinyanga ambapo shule kutoka halmashauri sita za wilaya mkoa huo zimeshiriki. 


Akifunga Mashindano hayo leo Jumanne June 11,2019,katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga Msovela alisema hataki kuona wanafunzi kutoka Shinyanga wanashiriki mashindano ya UMITASHUMTA 2019 kitaifa mkoani Mtwara,bali anataka vijana hao wakarudi na makombe ya kutosha. 

“Nataka mkalete makombe badala tu ya kuwa washiriki wa mashindano ya UMITASHUMTA kitaifa,naamini kabisa vijana wetu wameandaliwa vya kutosha na tutachagua kikosi imara kitakachotuletea ushindi katika mkoa wetu”,alisema Msovela. 

Aidha aliwataka wanafunzi watakaokwenda kushiriki mashindano hayo kitaifa kuwa na nidhamu ya kutosha na wakaoneshe vipaji vyao huku akiwakumbusha kuwa michezo ni ajira. 

Kwa upande wake,Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Dedan Rutazika alisema ili kuleta ushindi wa kishindo,wataunda timu ya ushindi yenye vipaji maalum. 

Rutazika aliitaja miongoni mwa michezo iliyokuwepo wakati wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019 yaliyofunguliwa mkoani Shinyanga Mei 27,2019 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack kuwa ni mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana,netiboli,riadha,riadha maalumu iliyohusisha watoto wasiosikia (viziwi),Goalball (kwa wasioona),ngoma na kwaya. 

Aliongeza kuwa washindi katika michezo yote wamejipatia zawadi ya makombe huku akiwataja washindi wa jumla kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na washindi mpira wa miguu kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Msalala,Usafi Manispaa ya Shinyanga,Riadha Shinyanga,pete/netiboli Manispaa ya Shinyanga.

Kauli mbiu ya Mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2019 ni 'Michezo na sanaa kwa elimu bora na ajira'.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela (katikati) akizungumza wakati wa kufunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA – 2019) mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage leo Juni 11,2019. Kulia ni  Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Dedan Rutazika,kushoto ni Afisa Michezo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Joseph Bihemo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akizitakia mchezo mwema timu zilizofuzu fainali mashindano ya UMITASHUMITA 2019 mkoa wa Shinyanga ambazo ni Halmashauri ya Msalala (jezi rangi ya machungwa) na Halmashauri ya wilaya ya Kishapu (jezi za bluu).
Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Dedan Rutazika akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya UMITASHUMTA 2019 mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akisalimiana na kuwakagua wachezaji wa timu ya Kishapu.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akisalimiana na kuwakagua wachezaji wa timu ya Msalala.
 Kikosi cha timu ya Kishapu
Kikosi cha timu ya Msalala.
Mtanange kati ya Msalala na Kishapu ukiendelea ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika hakuna aliyefanikiwa kuona lango la mwenzake wakalazimika kwenda kwenye matuta na timu ya Msalala kuibuka na ushindi wa magoli 5 -4.
Vijana wakishangilia uwanjani.
Mchezaji wa timu ya Kishapu akiipatia goli timu yake.
Mbwembwe zikiendelea uwanjani.
Golikipa wa timu ya Kishapu akitapatapa na shuti kali lilisukumwa na mchezaji wa Msalala.
Walimu na wanafunzi wa Msalala wakishangilia baada ya kuichapa Kishapu magoli 5 -4.
Mchezo wa fainali kati ya timu ya wasichana ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi nyeupe) na halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (jezi za bluu) ukiendelea.
Mchezo wa fainali kati ya timu ya wasichana ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi nyeupe) na halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (jezi za bluu) ukiendelea ambapo Manispaa ya Shinyanga waliibuka washindi kwa kuifunga Kishapu magoli 18 - 11.
Mchezo wa mpira wa netiboli kati ya timu ya wasichana halmashauri ya Kahama Mji na Msalala ukiendelea. Kahama Mji walipata magoli 20 huku Msalala ikipata magoli 19.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu wasichana kati ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi za bluu) na  Halmashauri ya Shinyanga wakisalimiana kabla ya mchezo.
Mchezo kati ya timu ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi za bluu) na  Halmashauri ya Shinyanga ukiendelea ambapo Halmashauri ya Shinyanga waliichapa Kishapu bao 1-0.
Mashabiki wa Halmashauri ya Shinyanga wakishangilia kwa kuichapa Kishapu bao 1-0.
Mashabiki wa mpira wakiwa uwanjani.
Wanafunzi wakiwa uwanjani.
Vijana wakishangilia timu zao.
Shangwe zikiendelea uwanjani.
Vijana wakicheza muziki uwanjani.
Vijana wakisubiri kupewa zawadi ya makombe.
Vijana wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa uwanjani.
Meza kuu wakiwa wamesimama tayari kwa kugawa zawadi kwa washindi wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019 mkoa wa Shinyanga.
Zoezi la utoaji zawadi ya makombe likiendelea : Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Dedan Rutazika akikabidhi zawadi ya makombe kwa washindi katika michezo yote. Washindi wa jumla kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na washindi mpira wa miguu kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Msalala,Usafi Manispaa ya Shinyanga,Riadha Shinyanga,pete/netiboli Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la utoaji zawadi ya makombe likiendelea : Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Dedan Rutazika akikabidhi zawadi ya makombe kwa washindi katika michezo yote. Washindi wa jumla kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na washindi mpira wa miguu kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Msalala,Usafi Manispaa ya Shinyanga,Riadha Shinyanga,pete/netiboli Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la utoaji zawadi ya makombe likiendelea 
Zoezi la utoaji zawadi ya makombe likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi ya makombe likiendelea. 
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527