TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, June 22, 2019

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI

  kisesa       Saturday, June 22, 2019


Inter Milan wanataka kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, 26, lakini watalazimika kumuuza mshambuliaji wao wa sasa Muargentina Mauro Icardi,26 kufadhili mkataba wa Lukaku. (Guardian)
Real Madrid wanampango wa kumnunua Paul Pogba kutoka Manchester United msimu huu wa joto kabla ya kumsaini mchezaji nyota wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Goal)

Tottenham watamchukua winga wa Uhispania wa miaka 22 Marco Asensio kama sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa Eriksen kwenda Madrid . (Sun)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameiambia klabu hiyo itamuuza Pogba kwa klabu itakayoweka dau kubwa zaidi, japo Juventus wameonesha nia ya kutaka kumnunua. (Star)Paul Pogba na Ole Gunnar Solskjaer

Tottenham inatarajia Juventus itaweka dau la kumnunua beki wa kulia Kieran Trippier, 28, na wako tayari kumuuza kiungo huyo wa kimataifa kwa karibupauni milioni 25. (Telegraph)

Paris St-Germain wameiambia Barcelona kuwa hawamuuzi Neymar, 27 kwa udi na uvumba. (Mail)

Real Madrid wanampango wa kusaini Ian Kylian Mbappe,26 kutoka PSG msimu ujao lakini wanataka mchezaji huyo raia wa Ufaransa kutoa ombi la kutaka uhamisho. (AS)Neymar (kushoto) na Kylian Mbappe

Atletico Madrid wanamtaka beki wa Arsenal Mhispania Hector Bellerin, 24, na wako tayari kumwachilia winga Vitolo, 29, kama sehemu ya mkataba wa usajili wake. (Telegraph)

Chelsea hawajaamua kumuuza mlinzi wao Mfaransa Kurt Zouma, 24, kwa Everton hadi watakapopata kocha mpya. (Star)

The Blues wanajiandaa kuilipa Derby pauni milioni 4 zinazohitajika kutimiza masharti ya mkataba wa Frank Lampard kabla hawajakamilisha mchakato wa kumuajiri kama kocha wao mpya wiki ijayo. (ESPN)

Chelsea wamempatia kipa Petr Cech la nafasi ya kitengo cha ufundi na mshauri wa michezo wakiwa na matumaini kuwa atashirikiana kwa karibu na Lampard. (Guardian)Petr Cech

Klabu ya Shanghai Greenland Shenhua kutoka China imetoa ofa ya pauni milioni 17.8 kumnunua Willian, 30, lakini mchezaji huyo wa Brazil huenda asikubali kujiunga nao kwasababu bado anataka kusalia Chelsea. (UOL Esporte, via Metro)

Mpango wa Arsenal wa kumnunua winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco au mshambuliaji wa Bournemouth Ryan na Uskochi Fraser huenda umekwama. (Evening Standard)

Meneja mpya wa Juventus Maurizio Sarri amesema hana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 27, kutoka Chelsea. (Sun)Jorginho

CHANZO.BBC SWAHILI
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post