TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA


Juhudi za kocha Ole Gunnar Solskjaer kuimarisha kikosi chake huenda zikagonga mwamba kwa sababu Manchester United ni klabu ambayo hutoa ofa ya chini kwa wachezaji wanaotaka kuwasajili. (Evening Standard)

Solskjaer anataka kumuuza kiungo wa kati wa Man Utd Mfaransa Paul Pogba, 26, bada ya kufahamishwa kuwa ana pauni milioni 100 ya kuwasajili wachezaji wapya msimu huu. (Star)

Mchezaji nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, hana mpango wa kuchezea tena Paris St-Germain. (Sport - in Spanish)

Real Madrid wameweka dau la euro milioni 130 kumnunua Neymar, kutoka PSG, mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, au mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Atletico Madrid wanakaribia kukamilisha usajili wa Joao Felix wa Benfica kwa kima cha euro milioni 120 sawa na (£106.7m) hii ina maanisha Manchester United watamkosa kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno aliye na umri wa miaka 19. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Mhispania Rodri, ameamua kujiunga na Man City badala ya Bayern Munich na kuhamia City kawa malipo ua £62m. (Kicker - in German)

Manchester City wanapigiwa upatu kuipiku Man Utd katika usajili wa Harry Maguire, 26, kutoka Leicester kwa kima cha pauni milioni 65 baada ya kiungo huyo wa England kupita vipimo vya matibabu. (Star)
Man City wanatafakari uwezekano wa kumsaini kwa mkataba wa bure Asier Riesgo wa ibar na kumfanya Mhispania huyo wa miaka 35 kuwa kipa wao wa tatu. (Manchester Evening News)

Everton wameanza maungumzo na Chelsea kuhusu usajili wa Kurt Zouma kwa mkataba wa kudumu baada ya mlinzi huyo wa Ufaransa, 24, kucheza Goodison Park msimu uliopita kwa mkopo katika. (Telegraph)

Tottenham wamefanya mazungumzo na ajenti wa kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24, kuhusu uhamisho wake kutoka Sporting Lisbon. (Telegraph)Bruno Fernandes

Juventus wanamatumaini ya kufukia mkataba wa kumsaini Adrien Rabiot kutoka Paris St-Germain, huku mkataba wa mchezaji huyo raia wa Ufaransa anaechezea safu ya kati ukitarajiwa kukamilika msimu huu wa joto. (Goal)

Liverpool hawana mpango wa kumuuza Divock Origi msimu huu wa joto licha ya mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mweye umri wa miaka 24 kusalia na mkataba wa mwaka mmoja. (Liverpool Echo)

CHANZO.BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527