SERIKALI YASEMA JUKUMU LA KULINDA WATOTO NI LA WAZAZI NA JAMII NZIMA


SALVATORY NTANDU
Serikali mkoani Shinyanga  imesema kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto unachangiwa na  wazazi/wazazi kutotimiza wajibu wao katika malezi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Kahama ANAMRING MACHA katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa afrika ambayo kimkoa imefanyika wilayani kahama na kusema kuwa wazazi wamejitoa katika malezi na kusababisha kuongezeka kwa matukio hayo.

Amesema Watoto wengi katika jamii wanakosa malezi kutokana kuwepo kwa dhana kuwa jukumu hilo lipo kwa serikali hali ambayo inasababisha watoto kukosa haki zao za msingi ikiwemo elimu,afya, chakula na malazi bora.

MACHA amefafanua kuwa Jukumu la kumlinda mtoto ni la mzazi/mlezi na jamii kwa ujumla hivyo ni budi wakatimiza wajibu wao ili kuhakikisha watoto wanatimiza malengo yao na kutokomeza vitendo vya ukatili kwa kundi hilo muhimu.

Sanjari na hilo             macha amesema  kuwa, wazazi wamekuwa chanzo cha kuwakwamisha watoto wao katika kutimiza ndoto zao hasa wanafunzi wakike kwa kuwaozesha wakiwa na mri mdogo ambao anahitajika kuwa shuleni nakuongeza serikali haitavumilia vitendo hivyoa ambavyo vimekuwa vinafanywa na wazazi wasiowadilifu.

Nae        Mwenyekiti wa baraza la watoto Mkoa Shinyanga VICTORY CHACHA Wakati akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wa mkoani humo amesema kuwa,upungufu wa walimu wa masomo ya hesabu na sayansi ndio imekuwa chanzo cha kushusha ufaulu wa wanafunzi.

Amefafanua kuwa  kuwa,wazazi na walezi wamekuwa na tabia ya kuwafungia watoto kike na wakiume walemavu na kuwanyima frusa ya kusoma kwa kuwa na imani potofu kuwa watachekwa kwenye jamii,nakuomba serikali kuliingilia jambo hilo kati ili kila mmoja awe kupata elimu bila kujali matabaka.

Mwisho


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post