RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UJENZI WA DARAJA LA BAHARINI


Rais John Magufuli hapo jana aliembelea mradi wa ujenzi wa daraja linalokatiza baharini kwa kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.

Rais Magufuli ameshuhudia shughuli za ujenzi zikiendelea vizuri ambapo mkandarasi ambaye ni kampuni ya GS Engineering ya Korea anakamilisha kuunganisha daraja la muda litakalomwezesha kuanza ujenzi wa nguzo za daraja.

Akiwa katika Rais Magufuli amekutana na Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Yooshin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee na kumuelezea kufurahishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo linatarajiwa kusaidia kupunguza msongamano wa magari kutoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Naye Suk-Joo Lee ameelezea kufurahishwa kwake kufanya kazi Tanzania na ameahidi kuwa kazi hiyo itakwenda vizuri.

Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1.03 na barabara za kuunganisha zenye urefu wa kilometa 6.23 na utagharimu takribani shilingi Bilioni 255. Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge na litarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2021.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527