RC MONGELLA AZINDUA RASMI MATUMIZI YA MIFUKO MBADALA "BEI ITASHUKA"


Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akionyesha mifuko mbadaya ambayo ni rafiki kwa mazingira inayopaswa kutumika.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye zoezi la kuhamasisha katazo la Serikali kuhusu uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko (vibebeo) ya plastiki kuanzia leo Juni 01, 2019.

Mongella ametumia fursa hiyo kuwatoa hofu wananchi wanaodhani inauzwa kwa gharama kubwa akisema nayo itashuka bei kama ilivyokuwa mifuko ya "Rambo" ambayo wakati inaanza kutumika ilikuwa ikiuzwa kwa gharama kubwa na baadae ikashuka.

Zoezi hilo limefanyika katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza na kwenda sambamba na uzinduzi rasmi wa matumizi ya mifuko mbadala ambapo wananchi na wafanyabiashara wamehimizwa kuendelea kusalimisha mifuko ya plastiki katika ofisi mbalimbali ikiwemo Serikali za Mitaa.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi amewahimiza wananchi wa Wilaya hiyo kuwa watiifu kutekeleza katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki na kutumia mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha amesema utekelezaji wa zoezi hilo utazingatia sheria hivyo wananchi waondoe hofu kwani zoezi hilo halitamuonea mtu yeyote na kwa wale ambao bado wana mifuko ya plastiki waendelee kuipeleka katika ngazi husika kama ilivyoelekezwa.
Afisa Mkaguzi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Abel Sembeka akizungumza wakati wa zoezi hilo ambapo amesema matumizi ya mifuko ya plastiki iliyozuiliwa ni ile inayohusisha vibebeo kama vile "Rambo" na kwamba mifuko ya plastiki ya vifungashio kama karanga, binzari na miwa bado haijazuiliwa.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana, akitoa salamu zake kwenye zoezi hilo ambapo amesema Serikali itasimamia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kuzingatia sheria hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya Serikali yao sikivu.
Viongozi mbalimbali mkoani Mwanza wakifuatilia zoezi la kuhamasisha katazo la Serikali kuhusu uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko (vibebeo) ya plastiki.
Wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wakifuatilia zoezi hilo.
Wadau wakiwa kwenye zoezi hilo.
Viongozi wa dini, wafanyabiashara wadogo na wananchi wakifuatilia zoezi hilo.
Wananchi na viongozi mbalimbali wa dini wakinyoosha mikono kuunga mkono katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akionyesha mifuko mbadaya ambayo ni rafiki kwa mazingira inayopaswa kutumika.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya viongozi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akimsikiliza mmoja wa akina mama wanaouza mifuko mbadala jijini Mwanza ambapo Mongella amesema baada ya muda mfupi ujao, mifuko hiyo itaanza kuuzwa kwa gharama nafuu baada ya wafanyabiashara wakubwa kumaliza taratibu za kuitoa bandarini.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya wananchi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.
Meneja wa kiwanda cha Falcon kilichopo jijini Mwanza akionyesha baadhi ya bidhaa ikiwemo mbao zinazotengenezwa kwa kutumia mifuko ya plastiki ambapo amewahamasisha wananchi kukusanya mifuko hiyo na kwenda kuiuza kiwandani hapo badala ya kuitapanya ovyo na kuharibu mazingira.
Baadhi ya wajasiriamali wakisalimisha mifuko ya plastiki kwenye zoezi hilo ambapo kampuni ya kufanya usafi ya GreenWestPro ilitumia zoezi hilo kuhamasisha wananchi na wafanyabiashara kusalimisha mifuko ya plastiki.
Zoezi la kusalimisha mifuko ya plastiki likiendelea jijini Mwanza.
Wananchi wameshauriwa kusalimisha mifuko ya plastiki katika ngazi husika ikiwemo ofisi za Serikali za Mitaa badala ya kuitapanya ovyo na hivyo kuhatarisha mazingira.
Kampuni ya GreenWestPro ni mdau mkubwa wa mazingira ambapo inafanya shughuli zake za usafi na utunzaji wa mazingira katika majiji matatu nchini ambayo ni Dar es salaam, Mwanza na Dodoma.
Kampuni ya GreenWastePro imetumia fursa hiyo kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya mifuko (vibebeo) ya plastiki na kujikita kwenye matumizi ya mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post