MNYETI: SINA NIA YA KUMDONDOSHA YEYOTE

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, amesema hana nia wala lengo la kumdondosha mtu kwenye yeyote nafasi yake kwa sababu hiyo siyo kazi yake.

Ametoa kauli hiyo jana Juni 28, katika kikao cha baraza la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Babati cha kujadili na kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo amesema yeye anashugulika na maendeleo ya watu wa Manyara.

“Sina nia wala lengo la kumdondosha mtu kwenye nafasi yake kwa sababu hiyo sio kazi yangu kama mtu anaona dalili za kushindwa asitafute sababu ya kinga kwamba Mnyeti ndiye anayenishughulikia mimi sishughuliki na mtu labda ukanyage waya wakati nahangaika na maendeleo hapo maana yake tutalipuana lazima shoti itokee,” amesema Mnyeti.

“Mimi nikiwa nahangaika na shida za wana Manyara wewe kaa pembeni, nikikushirikisha sawa nisipokushirikisha niache niendelee, ninapohangaika na shida za watu wa Manyara halafu wewe unakuja mbele kuziba lazima nitakufyatua,” amesema Mnyeti.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Babati Nicodemus Tarmom amesema muda uliopo ni wa kuchapa kazi na amemuomba mkuu wa mkoa aendelee kuwasaidia na wao watamsaidia kuona kazi yake inafanikiwa.

Na Beatrice Mosses – Manyara

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post