MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NDANI YA CHUMBA CHA MPENZI WAKE | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, June 30, 2019

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NDANI YA CHUMBA CHA MPENZI WAKE

  Malunde       Sunday, June 30, 2019
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta Felix Otieno  ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya nyumba ya mpenzi wake mtaani Ruiru nchini Kenya leo Jumapili Juni 30,2019.

Maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha Elite Special Prevention Unit wanashirikiana na polisi kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo.

 Imeripotiwa kuwa Otieno aliuwawa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati mpenzi wake hakuwa nyumbani.

 Marafiki aliokuwa na chumbani waliweza kutoroka bila ya kupatwa na majeraha, Otieno alikimbizwa hospitalini ila aliaga dunia kabla ya kuhudumiwa na madaktari.

Akidhibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa polisi wa Ruiru James Ngetich alisema uchunguzi umeanzisha ili kuwakamata waliohusika na mauaji hayo. 

" Tunafanya uchunguzi kubaini hao majambazi walikuwa akina nani na mbona walimlenga Otieno tu, madai mengi yameibuka ila hatutaki kubahatisha," Ngetich alisema kama alivyonukuliwa na gazeti la The Standard.

Chanzo - Tuko.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post