WANAODAIWA KUWA MAJAMBAZI WAUAWA MKOANI NJOMBE


Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi mkoani Njombe kwa kushirikiana na wananchi  limefanikiwa kuwaua watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi huku mmoja akifanikiwa kutoroka kwa kutumia gari  ndogo aina ya special.
Akizungumza na vyombo vya habari makao makuu ya jeshi hilo mjini Njombe kamishna msaidizi wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Salum hamduni amesema watu hao wameuawa kwa kujaribu kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha mjini makambako mkoani Njombe.

“Mnamo tarehe 5/6/2019 majira ya saa 20:15 katika kituo cha kuuza mafuta kiitwacho Negelo kilichopo mtaa wa kipagamo kata ya Makambako,watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi jinsia ya kiume wenye umri kati ya 35-45 waliuawa wakati wa bajibizano na askari polisi wakati walipovamia katika kituo hicho kwa lengo la kufanya unyang’anyi”alisema kamanda

Aidha kamanda wa polisi amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na walinzi wa kituo hicho cha mafuta waliweka mtego ndipo majira hayo wakafika watu hao wakiwa na gari dogo aina ya special wakiwa wamezima taa huku wakiwa wameshika silaha ndogo kila mmoja.

“Lakini watu hawa walipo amriwa na askari walikaidi amri hiyo na kuanza kufyutua risasi ndipo askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwaua majambazi wawili na katika eneo la tukio kumekutwa na silaha aina mbili za shotgun/gobore ikiwa na risasi 10,kisu kimoja,bisibisi moja, tiketi mbili za kusafiria kutoka Iringa hadi Makambako kwa kutumia basi la Lutengano,bangi misokoto minne,karatasi rizila na nguo mbali mbali za watu hao”aliongeza kamanda.

Aidha jeshi hilo limesema miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika hospital ya mji wa Makambako kwa uchunguzi,huku pia jeshi hilo likiendelea na upelelezi wa kumtafuta jambazi moja ambaye alikimbia katika eneo la tukio.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post