KUAHIRISHWA KWA ZOEZI LA AJIRA ZA WATUMISHI WA MUDA KWA AJILI YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa tarehe 30 Mei, 2019 iliwatangazia nafasi za kazi za muda kupitia tovuti yake ya www.nec.go.tz na kuwaalika watanzania wenye sifa zilizo ainishwa kwenye tangazo hilo kuomba nafasi hizo za kazi.

 
Hivyo, Tume inapenda kuwataarifu wananchi wote ya kwamba mchakato wa ajira za muda kwa ajili ya zoezi hilo umeahirishwa hadi hapo itakapotangazwa tena.

Aidha, Tume inapenda kutoa shukrani zake kwa wale wote walioleta maombi yao ya kazi na inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Dkt. Athumani Kihamia
MKURUGENZI WA UCHAGUZI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post