KOREA KASKAZINI YAITAKA KOREA KUSINI KUACHA KUWA MPATANISHI KATIKA MAZUNGUMZO YAO NA MAREKANI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 28, 2019

KOREA KASKAZINI YAITAKA KOREA KUSINI KUACHA KUWA MPATANISHI KATIKA MAZUNGUMZO YAO NA MAREKANI

  Malunde       Friday, June 28, 2019
Korea Kaskazini imeitaka Korea Kusini kusitisha juhudi zake za upatanishi katika mazungumzo yake na Marekani. 


Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na kiongozi wa Korea Kusini Moon Jae In mjini Seoul Jumapili baada ya mkutano wa kilele wa G20 huko Osaka Japan. 

Moon amesema Korea Kaskazini na Marekani wanatafakari kuandaa mkutano wa kilele kwa mara ya tatu. 

Mkutano wa pili kati ya Trump na Kim huko Hanoi mwezi Februari uliishia bila makubaliano kuhusiana na Korea Kaskazini kuharibu silaha zake za nyuklia ili ipunguziwe vikwazo. 

Lakini sasa mkurugenzi mkuu katika idara inayohusika na masuala kuhusu Marekani katika Wizara ya Mambo ya nje ya Korea Kaskazini Kwon Jong Gun amesema uongozi wa Korea Kusini ni bora ukashughulika na mambo yake ya ndani.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post