Picha : VIJANA WA KAMBI YA ARIEL WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI VYA IPP ,MAKUMBUSHO YA TAIFA DAR


Watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Simiyu,Mwanza,Mara na Shinyanga wanaoshiriki Kambi ya Ariel 2019 leo Juni 27,2019 wametembelea Vyombo vya Habari vinavyomilikiwa na Kampuni ya IPP Media ambavyo ni ITV,Radio One, Capital Radio,Capital Tv,East Africa Tv ili kujifunza namna wanavyoendesha vipindi na kurusha matangazo.

Vijana na watoto hao pia wametembelea Makumbusho ya Taifa ili kujifunza historia ya mwanadamu na nchi ya Tanzania pamoja na kiwanda cha kutengeneza juisi kinachomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa ili kujionea namna uzalishaji unavyofanyika.

Ziara hiyo inakuja baada ya watoto hao wanaoshiriki kambi ya Ariel 2019 ya wiki moja iliyoanza Juni 23,2019 jijini Dar es salaam, kujifunza darasani masuala ya VVU/UKIMWI, kukua, ujinsia,ujasiriamali na kujengewa ujasiri na kujiamini ili waweze kutimiza ndoto zao.

Kambi ya Ariel 'Ariel Camp' inasimamiwa na asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) ambayo inafanya shughuli zake katika mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Simiyu na Mara.

ANGALIA PICHA MATUKIO WAKATI WA ZIARA YA VIJANA NA WATOTO 
Kulia ni Mkurugenzi wa Radio One Stereo na Capital Radio ,Deogratius Rweyunga akiwaelezea vijana na watoto kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza na Mara wanaoshiri Ariel Camp 2019 namna wanavyoendesha vipindi vya radio. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa Radio One Stereo na Capital Radio,Deogratius Rweyunga akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu namna wanavyoendesha vipindi vya radio. Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Radio One Stereo Bahati Alex akifuatiwa na Mtangazaji wa kipindi cha Yaliyomo Yamo, Hatya Omary.
Mtangazaji wa kipindi cha Yaliyomo Yamo, Hatya Omary akiendelea na kipindi wakati vijana na watoto wa Ariel Camp 2019 walipotembelea studio ya Radio One.
Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa asasi ya AGPAHI,Agnes Kabigi akielezea 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo' lengo la ziara ya vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019.
Meneja Mawasiliano wa asasi ya AGPAHI,Agnes Kabigi akizungumza 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'. Kabigi alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kukaa na watoto na kuwaeleza kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI.
Kijana akielezea kuhusu VVU na UKIMWI 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'.
Kijana akielezea kuhusu VVU na UKIMWI 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'.
Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Capital Radio, Abdallah Mwaipaya akitoa ufafanuzi namna wanavyoendesha vipindi vya radio.
Hapa ni Control Room ITV: Kulia Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyoandaa vipindi vya Televisheni.
Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyofanya mawasiliano wakati wa kuandaa vipindi vya Televisheni.
Ndani ya chumba cha kurushia matangazo ITV na East Africa Tv: Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyorusha vipindi vya Televisheni.
Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akielezea namna wanavyofanya vipindi vya mahojiano ya vipindi mbalimbali.
Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akionesha namna kamera za studio zinavyofanya kazi.
Hapa ni chumba cha kusomea taarifa ya habari ITV: Kulia ni Fundi wa ITV, Paul Urio akiwaonesha vijana na watoto  namna wanavyoendesha vipindi vya habari.
 Fundi wa ITV, Paul Urio akiwaelezea vijana na watoto  namna wanavyoendesha vipindi vya habari.
Vijana na watoto wakipiga picha na Mtangazaji wa Kipindi cha Habari za saa, Richard Stephen.
Mtangazaji wa ITV ,Isaack Mpayo akielezea namna wanavyoendesha kipindi cha habari za saa.
Washiriki wa Ariel Camp 2019 wakiwasili katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya historia ya mwanadamu na historia ya nchi ya Tanzania.
Afisa Elimu Mwandamizi katika Makumbusho ya taifa,Anamery Bagenyi (aliyevaa nguo nyeupe) akielezea historia ya Makumbusho ya taifa yaliyoanzishwa mwaka 1940. Alisema katika Makumbusho hayo kuna maeneo matano ya kujifunza ambayo ni Chimbuko la Mwanadamu,jumba la maonesho ya kihistoria,jumba la michoro ya mapangoni na miamba,jumba la sanaa za kisasa,jumba la kumbukumbu ya ubalozi wa Marekani na Jumba la Baiolojia.
Afisa Elimu Mwandamizi katika Makumbusho ya taifa,Anamery Bagenyi (aliyevaa nguo nyeupe) akielezea historia ya Makumbusho ya taifa yaliyoanzishwa mwaka 1940.
Kushoto aliyenyoosha mkono ni Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Samson Yohana akionesha gari (la kijani) la kwanza kutumiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya Taifa,Samson Yohana akionesha moja ya nyumba za kihistoria.
Vijana na watoto wakipiga picha ya pamoja nje ya jumba la makumbusho lililojengwa mwaka 1940 na Waingereza.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Samson Yohana simba aliyekaushwa.
Vijana na watoto wakiwa katika jumba la makumbusho ya kihistoria.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha michoro mbalimbali katika jumba la sanaa za kisasa.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha michoro iliyochorwa mapangoni.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha vinyago.
Vijana na watoto wakiendelea kutembelea jumba la sanaa za kisasa.
Vijana na watoto wakifurahia kinyago cha mwanamke anayetwanga vitu huku kabeba mtoto na kashikilia mtoto.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha vitu mbalimbali vya asili.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha nyayo za binadamu wa kale.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha picha ya binadamu aliyejitambua.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Happiness Lema akitoa ufafanuzi kwa vijana na watoto kuhusu nyumba za historia.
Watoto wakisoma vitabu na kuangalia katuni kwenye vifaa vya kisasa katika Maktaba ya watoto katika makumbusho ya taifa.
Watoto wakisoma vitabu kwenye Maktaba ya watoto katika makumbusho ya taifa.
Vijana wakisaga unga wa ulezi kwa kutumia mawe katika makumbusho ya taifa.
Vijana wakisaga unga wa ulezi kwa kutumia mawe katika makumbusho ya taifa.
Kijana akikata nyama kwa kutumia jiwe.
Zoezi la kufuma mkeka likiendelea.
Afisa Elimu Mwandamizi katika Makumbusho ya taifa,Anamery Bagenyi akipiga picha ya kumbukumbu na washiriki wa Ariel Camp 2019 baada ya kutembelea Makumbusho ya taifa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post